Saturday, April 3, 2010
KIKWETE AWAOMBA WAFANYA KAZI NCHINI WASITISHE MGOMO
RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewaomba wafanyakazi wote nchini kusitisha mgomo ambao wameuandaa kupitia shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi na kuwaahidi madai hayo yatafanyiwa kazi.
Rai hiyo ameitoa jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi ya kungea na wananchi kwa kupitia njia ya vyombo vya habari vyfote nchini.
Ameitaka TUCTA kufikiri zaidi uamuzi huo na kusema mgomo huo utaathiri katika nyanja zote nchini.
Pia amekiri inamuwia vigumu kuzungumzia migomo hiyo kwa wakati na ameeleza kuwa serikali haipuuzi madai ya wafanyakazi wanawajali na wanawathamini.
Hivyo ameitaka TUCTA kukubali kufanya mazungumzo na serikali na waajiri wengine ili kumaliza mgogoro huo ambao hautajenga nchi bali itabomoa.
Mgomo huo unatarajiwa kuanza Mei 5, mweaka huu ambao unalenga mgomo wea wafanyakazi wote nchini kudai madai dambayo hayatekelezwi kwa muda mrefu na serikali.
Tayari vyama kadhaa vinavyounda shirikisho hilo vimeshatangaza kuunga mkono mgomo huo, ambao Kikwete amesema kama utafanyika "shughuli zote nchini zinazofanywa na watu walioajiriwa zitasimama kwa muda usiojulikana kuanzia siku hiyo".
TUCTA inataka siku hiyo watu wote walioajiriwa wagome na kwa muda usiojulikana. Tamko hilo linawahusu wafanyakazi wa umma serikalini na katika mashirika ya umma pamoja na wafanyakazi wa sekta binafsi walioajiriwa popote pale mashambani, maofisini, viwandani, majumbani, mahotelini na madereva.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment