Monday, March 22, 2010
MGOMO WA WAFANYA KAZI TANZANIA
SHIRIKISHO la Vyama vya wafanyakazi nchini {TUCTA] umetangaza mgomo utakaofanyika nchi nzima kuaninzia Mei 5, mwaka huu kupinga mambo mbalimbali serikalini. Nacho Chama cha Walimu Tanzania [CWT] umeunga mgomo huo na umesema utashiriki ipasavyo na wameheshimu kauli ya tucta kwa kuwa ina nguvu na wanakusudia kugoma hadi hapo haki zao zitakapotekelezwa ipasavyo.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kwa sasa anatoa taarifa kwa walimu wote nchini na wanatakiwa wafahamu kuwa chama chao kimeitikia wito wa kushiriki kwenye mgomo wa kudai mambo mbalimbali ambayo serikali imeyadharau kwa muda mrefu.
Aliongeza kuwa viongozi wa vyama vyote wamekubaliana kuwatangazia wanachama wao kuhusu mgomo huo ili washirikiane kudai haki zao chini ya mwavuli wa Tucta.
Mgomo huo unakusudia madai ya mishahara duni isiyokidhi mahitaji, mafao duni ya wastaafu kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na ulipishwaji wa kodi kubwa kwenye mishahara midogo wanayopata wafanyakazi.
Tucta imedai kuwa siku ya kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi Mei Mosi watajadili kindani jinsi ya kuanza kufanya mgomo huo kwa kuw wafanyakazi wote hukutana siku hiyo.

BIBI CINHTIA NI MWANAMKE ALIYEIBIWA MME WAKE AENDA KUSHTAKI MAHAKAMANI NAKULIPWA FIDIA YA DOLLA MILIONI 9
Mwanamke wa nchini Marekani aliyemfikisha mahakamani mwanamke aliyempora mumewe, ameshinda kesi aliyomfungulia mwanamke huyo kwa kumuibia mumewe na atalipwa fidia ya dola milioni 9. Cynthia Shackelford mwenye umri wa miaka 60 aliiambia mahakama ya North Carolina kuwa aliacha kazi yake ya ualimu ili kulea watoto na kumsaidia mumewe Allan katika kuziendeleza shughuli zake za kisheria.
Kwa kutumia kipengele cha sheria ambacho huwa hakitumiki sana, Bi Cynthia alisema kuwa mumwe alikuwa ni mtu mwenye furaha na mwenye kuonyesha mapenzi kwake kabla ya bi Anne Lundquist, 49, kuuingilia uhusiano wao na kuanza uhusiano na mumewe.
Baada ya siku mbili za kuisikiliza kesi hiyo, majaji waliamuru bi Cynthia alipwe fidia ya dola milioni 9 baada ya bi Cynthia kuithibitishia mahakama jinsi mapenzi yao yalivyokuwa motomoto kabla ya Anne kuanza uhusiano na mumewe.
Mahakama ilitaka bi Cynthia alipwe fidia kwa kitendo cha mumewe kutembea nje ya ndoa yao na kumuumiza kihisia bi Cynthia.
Anne ambaye hivi sasa anaishi na Allan, alisema kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo akidai kuwa alianza uhusiano na Allan baada ya ndoa ya Allan na mkewe kuvunjika.
Jimbo la North Carolina ni miongoni mwa majimbo machache ya Marekani ambayo yanaruhusu wanandoa kuwafikisha mahakamani wenzao wanaozisaliti ndoa zao.
A VICTORY FOR THE AMERICAN PEOPLE
The passage of health insurance reform legislation represents a historic victory for the American people. America's families and businesses will not only get relief from skyrocketing health care costs but will now have more control over their health care. No longer will the insurance companies get the final say when it comes to rates and rights.
Health Reform
- Reduce long-term growth of health care costs for businesses and government
- Protect families from bankruptcy or debt because of health care costs
- Guarantee choice of doctors and health plans
- Invest in prevention and wellness
- Improve patient safety and quality of care
- Assure affordable, quality health coverage for all Americans
- Maintain coverage when you change or lose your job
- End barriers to coverage for people with pre-existing medical conditions
Health Reform & the Budget
“Under this budget, we will provide the health and human services that Americans depend on more effectively, slashing waste and focusing programs on results.”
-- Secretary Sebelius
The President’s budget helps build the foundation for health insurance reform. The budget strengthens the health care system and improves access to care by investing $995 million to address the shortage of health care providers in underserved areas, increasing funding to expand services at Health Centers by $290 million and allocating nearly $80 million for work to spread the adoption and use of health information technology.
ASKOFU KAKOBE BADO VITANI NA SERIKALI
kuonesha Serikali ipo katika juhudi za kuboresha huduma za nishati ya umeme nchini, jana mabango la Kanisa la Full Gospel Fellowship linaloonyehsa na kuwaelekeza watu kufika kanisani hapo limetolewa na mafundi wa Tanesco chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mabango hayo mawili yalisimikwa nje ya kanisa la Full Gospel Bibilia Fellowship(FGBFC) Linaliongozwa na askof Zakaria kakobe Jijini Dar es Salaam.
Mbali na kuondolewa mabango hayo pia askofu huyo ametakiwa na serikali kwa kupitia wakala wa barabara nchini (TANROAD)kuwajibika kulipa gharama za uondoaji wa mabango hayo kutokana na kuchelewa kufanya kazi hiyo kama alivyoelekezwa'
Mabango hayo yaliondolewa baada ya kudai kuwa mabango hayo yapo kwenye njia ya mradi wa umeme wa magawati 1332 na ni lazima yangetolewa kupisha mradi huo na kanisa hilo limetakiwa kuwajibika kulipa gharama hizo kwa kuwa yamechelewesha kazi ya utandazaji wa waya za umeme huo,amabapo kazi hiyo ilipangwakukamilika machi 15,mwaka huu.
Hata hivyo wakati kazi hiyo ukiendelea askofu kakobe na waumini wake hawakushiriki zoezi lake na walijifungia kanisani wakifanya maombi

MAKONTENA YA BIDAA BANDIA YAKAMAKWA BANDARINI DAR
Shehena ya makontena 20 za betri aina ya tiger head kutoka China zimekamatwa kutokana na kukosa ubora wa viwango vya matumizi ya bidaa hiyo.
Kontena hizo zimekamatwa katika operesheni ya Shirika la viwango nchini (TBS) katika kukagua bidaa ziingiazo nchini ambazo hazina viwango vya matumzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS nchini Charles Ekerege alisema shehena walioyakamata ya betri hizo ilifika nchini januari mwaka huu, lakini walipozikagua waligundua kuwa hazina ubora uliowekwa na shirika hilo.
Alisema betri hizo zinaingizwa nchini na wafanya biashara wakubwa na wakati mwingine imedaiwa kuwa wanaziingiza kwa njia ya panya.
Alisema betri hizo huingizwa nhini na huuzwa kwa bei za rejareja shilingi 350 na zinazotengenezwa hapa nchini huuzwa kwa shilingi 450 kila moja na watanzania wengu hukimbilia betri hizo kutokana na unafuu wa bei.
SKENDO ZA VATICAN
Papa Benedict XVI ametoa tamko rasmi la kuwaomba radhi wahanga wa skendo la wachungaji kuwalawiti na kuwanyanyasa kijinsia watoto waliokuwa wakienda kanisani. Skendo hilo limeyakumba makanisa ya kanisa katoliki katika nchi mbali mbali duniani lakini Ireland ndio iliyotajwa zaidi kwa idadi kubwa ya watoto walionyanyaswa kijinsia na wachungaji huku kanisa katoliki nchini Ireland likifunika maovu ya wachungaji wake ili kanisa lisiharibiwe sifa yake.
"Najua mmenyanyasika sana na kufanyiwa ukatili na nawaomba radhi sana wote waliokumbwa na maovu haya", alisema Papa katika taarifa yake kwa makanisa ya Ireland.
"Najua hakuna kitu kinachoweza kuuondosha uovu mliofanyiwa, Imani zenu kwa kanisa zimesalitiwa".
"Sote tumekumbwa na skendo linalotokana madhambi ya baadhi ya wadau wa kanisa".
"Madhambi makubwa yamefanyika dhidi ya watoto wasio na utetezi wowote".
"Najua baadhi yenu mnaona ni vigumu hata kuingia tena kwenye milango ya kanisa baada ya yote haya yaliyotokea", aliendelea kusema Papa Benedict.
Kwa miaka zaidi ya 10 wachungaji na viongozi wa kanisa wameharibu imani za watu ndani ya kanisa, alisema Papa katika taarifa yake ambayo itasomwa kwenye makanisa karibia yote nchini Ireland wakati wa misa ya jumapili.
Maskendo ya ngono yanayowahusisha wachungaji na watoto wa kiume yamekuwa yakiripotiwa katika nchi mbali mbali duniani huku nchi zilizokumbwa zaidi na maskendo hayo zikitajwa kuwa ni Austria, Uswizi, Uholanzi, Brazil, Mexico na hata dayosisi ya kanisa la zamani la Papa nchini Ujerumani imo kwenye skendo hilo.
Papa alisema kuwa miaka ya kuficha maovu ya wachungaji waovu imeisha na ametaka wachungaji watakaogundulika kuendeleza maovu yao waripotiwe polisi.
Papa aliongeza kuwa katika miaka iliyopita ameishakutana na baadhi ya wahanga wa skendo hilo kutoka nchi mbalimbali duniani na anatarajia kufanya hivyo tena baadae.
Subscribe to:
Posts (Atom)