WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Thursday, April 1, 2010

ATUPWA JELA MIEZI 6 KWA KUMUONYESHA MWARABU KIDOLE CHA KATI



Raia wa Uingereza anayeishi Dubai huenda akatupwa jela miezi sita kwa kosa la kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa kiarabu toka Iraq.
Simon Andrews, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 56 anakabiliwa na hukumu ya kwenda jela miezi sita iwapo atapatikana na hatia ya kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa urubani toka Iraq.

Gazeti la The Sun la Uingereza limeripoti kuwa Simon alishindwa kuzizuia hasira zake wakati wa ugomvi wake na mwanafunzi Mahmud Rasheed na kuamua kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati.

Mahmud alikimbilia polisi kupeleka malalamiko yake na haikuchukua muda mrefu Simon alitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mahakamani.

Simon amepigwa marufuku kusafiri nje ya Dubai tangia alipotiwa mbaroni mwezi wa nane mwaka jana.

Akitoa ushahidi wake mahakamani siku ya jumapili, Simon alijitetea kuwa hakufanya kitendo hicho na kwamba raia huyo wa Iraq anamsingizia.

Mahmud hakujitokeza mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Simon na pia hakuna mtu aliyejitokeza kama shahidi wa kesi hiyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi aprili nne wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

DUKA LA KWANZA LA NGONO LA KIISLAMU LAZINDULIWA UHOLANZI



Duka la kwanza la bidhaa za ngono zinazodaiwa kuwa ni 'HALAL' limezinduliwa kwaajili ya waislamu nchini Uholanzi na baadhi ya mashehe wametoa ruhsa ya duka hilo la kwenye internet wakisema kuwa halivunji sheria za kiislamu.
Duka hilo linalodaiwa kuwa duka la kwanza duniani kwaajili ya waislamu wanaohitaji bidhaa za kuchombeza mapenzi yao lilizinduliwa wiki iliyopita.

Ndani ya siku nne za kuzinduliwa kwa mtandao wa tovuti hiyo kulikuwa na jumla ya cliks 70,000, alitamba mmiliki wa tovuti hiyo ya kwanza ya bidhaa za ngono kwaajili ya waislamu, Abdelaziz Aouragh.

Tovuti hiyo inayoitwa "El Asira" kwa maana ya jamii katika lugha ya kiarabu, ilizinduliwa kwa lengo la kuwauzia wanandoa wa kiislamu bidhaa za erotika.

Abdelaziz ambaye ni raia wa Uholanzi mwenye asili ya Moroko alisema kuwa alianzisha duka hilo la kwenye mtandao ili kuwaepusha waislamu kuingia kwenye tovuti zinazouza bidhaa hizo ambazo huweka picha na video za ngono ambazo ni haramu katika uislamu.

Ukurasa wa mbele wa El Asira hauna kitu chochote zaidi ya mstari unaotenganisha wanawake na wanaume, wanawake hutakiwa kuclick upande wao wa kushoto na wanaume huingia upande wa kulia.

Tovuti hiyo ina lugha tatu za kidachi, kiarabu na kiingereza na huuza zaidi mafuta kwaajili ya masaji, mafuta ya kupunguza ukinzani (lubricants) na dawa mbali mbali za malavi davi.

"Kila kinachopatikana humu ni Halal kinaruhusiwa katika uislamu' alisema Abdelaziz na kuongeza kuwa hakuna picha wala video za ngono kwenye tovuti yake.

Tovuti hiyo inaonyesha bidhaa zikiwa zimepigwa picha kwenye maboxi yake.

Abdelaziz alisema kuwa kabla ya kuanzisha duka hilo la kwenye mtandao alipata ushauri toka kwa mashehe mbalimbali na wanazuoni wa Uholanzi na Saudia ambao walimwambia kuwa hakuna sheria ya kiislamu anayoivunja.

"Ili mradi hauzi toys za ngono au vitu kama hivyo, hakuna tatizo lolote", alisema imamu wa Uholanzi, Abdul Jabbar.

"Mtume Muhammad (s.a.w) alitoa ushauri mbalimbali kuhusiana na masuala ya mapenzi kwenye ndoa, hivyo hakuna kitu cha kukionea aibu", aliongeza imamu huyo.

KIKWETE AZINDUA JENGO LA UPASUAJI WA MOYO



RAIS Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi katika jengo la tiba la magonjwa ya upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Pia jengo hilo ni kituo cha mafunzo ya atiba ya magonjwa hayo nchini.

Udhamini wa Ujenzi huo umetokana na ahadi ya Rais Hu Jintao wa China, aliyoahidi kuisaidia Tanzania alipokutana na Rais Kikwete mwaka 2006 kwenye mkutano wa China-Africa jiji Beijing.

Kikwete alisema nchi ilikuwa inahitaji kwa miaka mingi kujenga kituo hicho na uwezo wa kutibu na kufanya upasuaji wa moyo nchini na sasa imeshukuru Rais Jintao kwa kujenga kituo hiko na Tanzani itakuwa imejikomboa katika changamoto hiyo.

Alisema nchi ilikuwa inatumia gharama kubwa sana za matumizi kusafirisha wagonjwa kuwapeleka nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji wa moyo.

Hivyo hatua hiyo ni chachu ya matumaini na inawapeleka wataalamu 26 kutoka nchini kwenda India kupata mafunzoya upasuaji, wakiwemo madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo wanne na madaktari wa moyo sita.

MWaka huu ilidaiwa kulikuwa na wagonjwa wapato 200 wa maradhi ya moyo na kati yao walioweza kubahatika kupelekwa nje ni 60 na wengine bado hawajapelekwa kutokana na gharama kuwa kubwa kuwatibu wagonjwa hao.

Hivyo kituo hicho kitaleta faraja ya nchi na Tanzania ditakuwea miongoni mwa nchi zitkazoweza kutibu magonjwa hayo.

VIDEO YA NYOTA WA MUZIKI MAREKANI AVUA NGUO HADHARANI



Erykah Badu katika video yake iliyosababisha mtafaruku
Mwanamuziki nyota wa Marekani, Erykah Badu ameingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya kuvua zake zote na kubakia uchi katika sehemu ambayo rais wa Marekani, John F Kennedy aliuliwa kwa risasi.
Nyota wa muziki wa R&B, Erykah Badu ameingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya kutengeneza video yake mpya ya muziki akivua nguo na kubakia uchi katika sehemu ambayo rais wa zamani wa Marekani, John F Kennedy alitunguliwa kwa risasi na kuuliwa.

Katika video yake hiyo mpya iliyochukuliwa mjini Dallas bila kibali wala ruhusa ya kujianika hadharani, Badu anaonekana akisaula nguo moja moja hadi kubakia mtupu wa mnyama na kisha kuigiza amepigwa risasi na kuanguka chini akijifanya amefariki.

Rais Kennedy alipigwa risasi na Lee Harvey mwaka 1963 wakati alipokuwa kwenye msafara wa magari ya rais pamoja na mkewe.

Badu ambaye alizaliwa Dallas mwaka 1971 ametoa albamu yake mpya inayoitwa "New Amerykah Part Two: Return of the Ankh".

Badu amesababisha mawazo tofauti toka kwa Wamarekani ambapo wengi wanasema kuwa ameidhalilisha sehemu ya kihistoria kwa kitendo chake hicho ambacho alikifanya mchana kweupe bila ya kujali kama kuna watoto au la.

Taarifa zinasema kuwa polisi huenda wakamkamata na kumtia mbaroni Badu kwa makosa ya kujianika hadharani.

Chini ni VIDEO ya Erykah Badu iliyozua kasheshe.


VIDEO – Nyota wa Marekani Avua Nguo Hadharani

MAITI ZA WATOTO ZATUPWA KWENYE MTO CHINA


Maiti za watoto zikiopolewa toka kwenye mto
Wafanyakazi wawili wa monchwari nchini China wanashikiliwa na polisi baada ya kuzitupa maiti 21 za watoto kwenye mto.
Wafanyakazi wawili wa ngazi za juu wa hospitali moja nchini China wamefukuzwa kazi huku wafanyakazi wawili wa monchwari wakiwa mbaroni baada ya maiti 21 za watoto kuopolewa toka kwenye mto.

Maiti za watoto wanane zilikuwa na alama za kuonyesha kuwa zilikuwa zimehifadhiwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Jining Medical University katika mji wa Shandong, limeripoti shirika la habari la Xinhua.

Taarifa zinasema kuwa maiti za watoto hao zilikuwa ni za vichanga vilivyouliwa wakati wa utoaji mimba na watoto waliofariki kutokana na maradhi mbali mbali.

Taarifa za polisi zinasema kuwa wafanyakazi hao wa monchwari walilipwa na ndugu wa watoto waliofariki wazizike maiti za watoto hao lakini wao waliamua kuzitupa kwenye mto ulio mbali sana na hospitali hiyo.

Maiti za watoto zikiwa katika mifuko ya rambo ya njano ziliopolewa toka kwenye mto na kuzua hasira za wananchi walioshuhudia tukio hilo.

Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.


VIDEO - Maiti za Watoto Zatupwa Kwenye Mto