WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Monday, April 19, 2010

APIGIWA KURA YA U MEAYA WAKATI WAMESHA FARIKI


Wapiga kura nchini Marekani wamemchagua mtu aliyefariki awe meya wao mpya.
Carl Geary alifariki mwezi mmoja uliopita kutokana na shambulio la moyo wakati akipiga kampeni za kuwania umeya wa mji mdogo wa Tracy City, Tennessee nchini Marekani.

Lakini pamoja na kwamba watu wengi walikuwa wakijua kuwa ameishafariki, marehemu Carl alishinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi sana mara tatu zaidi ya mpinzani wake.

Mjane wa marehemu Bi Susan Geary alisema kuwa matokeo ya uchaguzi hayamjashangaza kwani aliyatarajia.

"Siku aliyofariki watu walikuwa wakinipigia simu kutoa salamu za rambirambi wakisema kuwa watampigia kura kwenye uchaguzi".

Carl aliyefariki akiwa na umri wa miaka 55, alijulikana sana kwa misimamo yake thabiti ya kisiasa.

Pamoja na kwamba alishazikwa wiki kadhaa zilizopita, Carl alishinda uchaguzi kwa kupata kura 285 huku mpinzani wake akiambulia kura 85.

Mmoja wa wafanyabiashara katika mji huo alisema kuwa watu waliamua kumpigia kura Carl ili kuonyesha upinzani wao kwa meya aliyopo madarakani Bi. Barbara Brock.

"Nilikuwa nikijua kuwa ameishafariki, najua watu wataona kama ni upuuzi lakini tulitaka tupate meya mwingine sio huyu aliyepo", alisema Chris Rogers, mmiliki wa mgahawa mmoja uliopo mjini humo.

"Kama uchaguzi utarudiwa tena wiki ijayo nitampa kura yangu tena marehemu".

Maafisa wa mji huo wamesema kuwa manispaa itafanya kikao kuamua nani awe meya.

UREMBO WASABABISHA KIFO SIKU YA KUZALIWA KWAKE


Mwanamke wa nchini Uingereza aliyesherehekea kutimiza umri wa miaka 34 kwa kutoboa ulimi wake kuweka kichuma amefariki siku mbili baadae kutokana na sumu iliyotokana na kichuma hicho.
Amanda Taylor alipuuza kauli za familia yake kumpinga kuweka kichuma cha inchi moja kwenye ulimi wake na aliamua kuutoboa ulimi wake kuweka kichuma hicho ili kusherehekea kutimiza umri wa miaka 34.

"Kwa muda mrefu alifikiria kuutoboa ulimi wake kuweka kichuma", alisema mama yake Lorraine Taylor mwenye umri wa miaka 61.

"Siku nne kabla ya siku yake ya kuzaliwa aliniambia kuwa anataka kuweka kichuma kwenye ulimi wake siku ya kuzaliwa kwake", aliendelea kusema mama yake.

"Nilimpinga na kumuonya asifanye hivyo lakini alisema kuwa marafiki zake wote wameishaweka vichuma kwenye ndimi zao".

Kwa shingo upande mama yake alimpa ruhusa Amanda kutoboa ulimi wake lakini siku mbili baadae Amanda alikutwa nyumbani kwake akiwa amefariki.

Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa alifariki kutokana na damu yake kuingia sumu iliyotokana na kichuma alichowekewa kwenye ulimi wake.

Uchunguzi zaidi kuhusiana na kifo chake unaendelea.

VIDEO YA MUAFRICA TOKA TOGO ATENGENEZA ROBOT


Kusema ukweli waafrika Mungu katujalia akili nyingi sana lakini hali zetu duni za kiuchumi ndizo siku zote zinazoturudisha nyuma siku zote.
Angalia video ya mwanafunzi huyu wa nchini Togo ambaye kwa kutumia vifaa toka kwenye televisheni mbovu ameweza kutengeneza robot kama yale ambayo makampuni ya nchini Japan yamekuwa yakifanya utafiti kuyaboresha.

Sam Todo ambaye ni mwanafunzi wa nchini Togo alitumia vifaa toka kwenye televisheni mbovu na vifaa vingine vya umeme kuweza kutengeneza robot ambalo linaweza kutembea na kupunga mikono kwa kutumia remote control.


Bila shaka kijana kama huyu kama angeweza kupata vifaa vya kisasa au angepata mfadhili wa kukuza kipaji chake angeweza kufanya mambo makubwa kuliko haya.

Angalia video yake chini.


VIDEO - Waafrika Tupo Fiti Sana Basi tu..

SKENDO YA NGONO NDANI YA TIMU YA TAIFA UFARANSA



Skendo kubwa la ngono limeikumba timu ya taifa ya soka ya Ufaransa ambapo baadhi ya nyota wa timu hiyo ya taifa wanadaiwa kufanya mapenzi na machangudoa wenye umri mdogo.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa wamehusishwa kwenye skendo la kufanya mapenzi na makahaba wenye umri chini ya miaka 18.

Mchezaji nyota wa Ufaransa, Franck Riberry na Sidney Govou ni wachezaji wawili waliotajwa ambao tayari wameishahojiwa na polisi kuhusiana na skendo hilo.

Riberry anayeichezea Bayern Munich ya Ujerumani ana mke lakini naye amenaswa katika skendo hilo akidaiwa kufanya mapenzi na msichana kahaba mwenye umri chini ya miaka 18.

Taarifa zilisema kuwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus" walikuwa wakienda sana kwenye klabu moja ya starehe ya jijini Paris ambapo walikuwa wakiandaliwa makahaba wenye umri chini ya miaka 18. Mmoja wa makahaba hao inadaiwa alikuwa na umri wa miaka 14.

Wachezaji wengine nyota wa Ufaransa nao wamehusishwa na skendo hilo lakini majina yao yamewekwa kapuni.

Mmoja wa wachezaji hao alikiri kufanya mapenzi na msichana mwenye umri mdogo lakini alijitetea kuwa wakati huo alikuwa akiamini kuwa mwanamke aliyeletewa ni mtu mzima.

Kuwadi "Pimp" anayedaiwa kuwaandalia wachezaji machangudoa hao ametiwa mbaroni na baadhi ya wasichana hao wanaendelea kuhojiwa na polisi.

Skendo hilo limekuja ikiwa ni miezi miwili tu kabla ya Ufaransa kuja barani Afrika kwaajili ya fainali za kombe la dunia.

BINGWA WA ZAMANI WA NDONDI AJINYONGA


Bingwa wa zamani wa dunia wa ndondi za uzito mwepesi za mashirikisho ya ndondi ya WBC na WBA, Edwin Valero amejinyonga kwa kutumia nguo zake ikiwa ni masaa 48 baada ya kutupwa mahabusu kwa tuhuma za kumuua mke wake.
Edwin Valero, raia wa Venezuela ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa mashirikisho ya WBA na WBA katika uzito mwepesi, amejinyonga mwenyewe kwa kutumia nguo zake ndani ya selo ya polisi alipokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchomachoma na kisu.

Polisi walimtia mbaroni Valero siku ya jumapili baada ya kuukuta mwili wa mkewe Jennifer, 24, kwenye chumba cha hoteli moja mjini Valencia, Venezuela.

Valero alikuwa akitambulika kama shujaa wa Venezuela kutokana na rekodi yake nzuri kwenye ndondi. Alishinda mapambano yake yote 27 ya kimataifa kwa knockout.

Taarifa zinasema kuwa Valero mwenye umri wa miaka 28, aliondoka hotelini hapo majira ya alfajiri ya siku ya jumapili akiwaambia walinzi wa hoteli kuwa amemuua mke wake aliyezaa naye watoto wawili.

Valero inaripotiwa kuwa alikuwa na makosa kadhaa ya uvunjaji wa sheria. Alipigwa marufuku kuendesha gari nchini Marekani na mwezi uliopita alishtakiwa kwa kumshambulia mkewe na kisha kuwatishia maisha madaktari waliokuwa wakimpatia tiba mkewe.