Tuesday, June 1, 2010
Watanzania Kuzilipa Gharama za Kuwaleta Wabrazili
Washabiki wa soka Tanzania ndio wataolazimika kujipinda ili kuzilipa dola milioni 2.5 ambazo Brazili imelipwa ili kuileta timu yake Tanzania.
Shirikisho la soka Tanzania, TFF limepanga viingilio vikubwa kwenye mechi kati ya Brazili na Tanzania itakayofanyika jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam.
Viingilio vimekuwa vikubwa kuliko kawaida ili kulipia gharama za kuwaleta mastaa wa Brazili Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vingi vya habari, Tanzania imewalipa Brazili dola milioni 2.5 ingawa TFF imekataa kusema imewalipa Brazili dola milioni ngapi.
TFF ilisema kuwa kuwaleta Brazili nchini Tanzania ni gharama sana hivyo Watanzania wajiandae kukaza mikanda kulipa gharama hizo.
TFF inaamini kuwa mapato ya magetini yatatosha kuzilipa gharama za kuwaleta Brazili Tanzania.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa juni 7 vimepangwa kuanzia Tsh. 30,000 hadi Tsh. 200,000.
Majukwaa ya VIP tiketi zinaanzia laki moja hadi laki mbili ambapo taarifa za TFF zinasema kuwa tiketi za laki mbili zimeishanunuliwa zote.
Majukwaa yaliyobakia tiketi zinaanzia Tsh. 30,000 hadi Tsh. 80,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment