WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Monday, March 22, 2010

BIBI CINHTIA NI MWANAMKE ALIYEIBIWA MME WAKE AENDA KUSHTAKI MAHAKAMANI NAKULIPWA FIDIA YA DOLLA MILIONI 9


Mwanamke wa nchini Marekani aliyemfikisha mahakamani mwanamke aliyempora mumewe, ameshinda kesi aliyomfungulia mwanamke huyo kwa kumuibia mumewe na atalipwa fidia ya dola milioni 9. Cynthia Shackelford mwenye umri wa miaka 60 aliiambia mahakama ya North Carolina kuwa aliacha kazi yake ya ualimu ili kulea watoto na kumsaidia mumewe Allan katika kuziendeleza shughuli zake za kisheria.

Kwa kutumia kipengele cha sheria ambacho huwa hakitumiki sana, Bi Cynthia alisema kuwa mumwe alikuwa ni mtu mwenye furaha na mwenye kuonyesha mapenzi kwake kabla ya bi Anne Lundquist, 49, kuuingilia uhusiano wao na kuanza uhusiano na mumewe.

Baada ya siku mbili za kuisikiliza kesi hiyo, majaji waliamuru bi Cynthia alipwe fidia ya dola milioni 9 baada ya bi Cynthia kuithibitishia mahakama jinsi mapenzi yao yalivyokuwa motomoto kabla ya Anne kuanza uhusiano na mumewe.

Mahakama ilitaka bi Cynthia alipwe fidia kwa kitendo cha mumewe kutembea nje ya ndoa yao na kumuumiza kihisia bi Cynthia.

Anne ambaye hivi sasa anaishi na Allan, alisema kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo akidai kuwa alianza uhusiano na Allan baada ya ndoa ya Allan na mkewe kuvunjika.

Jimbo la North Carolina ni miongoni mwa majimbo machache ya Marekani ambayo yanaruhusu wanandoa kuwafikisha mahakamani wenzao wanaozisaliti ndoa zao.

No comments:

Post a Comment