
Shehena ya makontena 20 za betri aina ya tiger head kutoka China zimekamatwa kutokana na kukosa ubora wa viwango vya matumizi ya bidaa hiyo.
Kontena hizo zimekamatwa katika operesheni ya Shirika la viwango nchini (TBS) katika kukagua bidaa ziingiazo nchini ambazo hazina viwango vya matumzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS nchini Charles Ekerege alisema shehena walioyakamata ya betri hizo ilifika nchini januari mwaka huu, lakini walipozikagua waligundua kuwa hazina ubora uliowekwa na shirika hilo.
Alisema betri hizo zinaingizwa nchini na wafanya biashara wakubwa na wakati mwingine imedaiwa kuwa wanaziingiza kwa njia ya panya.
Alisema betri hizo huingizwa nhini na huuzwa kwa bei za rejareja shilingi 350 na zinazotengenezwa hapa nchini huuzwa kwa shilingi 450 kila moja na watanzania wengu hukimbilia betri hizo kutokana na unafuu wa bei.
No comments:
Post a Comment