Sunday, March 28, 2010
KAPUYA AWEKA UWAZIRI PEMBENI NA KUANZA KUPEKECHA
Katika hali isiyo ya kawaida kwa viongozi wa juu nchini kuonekana katika kumbi za starehe tena katika sare sambamba na waimbaji wa bendi, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya aliingia ukumbini na kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya wana wa Akudo. Huku akiwa amevalia sare sawa na waimbaji wa bendi ya Akudo, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya alijitosa ukumbini na kuanza kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya bendi ya Akudo Impact iliyokuwa ikitoa burudani kwenye ukumbi wa Msasani Beach.
Kapuya ambaye ndiye mmliki wa bendi hiyo alijimwaga stejini na kusakata muziki kwa nguvu zote huku jasho likimtoka akiwa pamoja na mpambe wake ambaye jina lake halikufahamika.
Kapuya anakuwa kiongozi wa pili wa juu serikalini kumiliki bendi wa kwanza alikuwa Waziri Mdhihiri Mdhihiri ambaye aliwahi kumiliki bendi ya Mchinga Sound ambayo baadaye ilivunjika.
Kutokana na jinsi anavyoithamini bendi yake, waziri Kapuya amefanikiwa kuifanya bendi ya Akudo iwe miongoni mwa bendi zinazopendwa sana nchini kiasi cha kuleta ushindani mkubwa katika medani ya muziki wa dansi hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment