
JESHI la polisi nchini lemefanikiwea kukamatwa majambazi 37 sugu katika operesheni inayoendelea nchi nzima.
Majambazi hayo yamekamatwa katika siku tofauti tofauti katika msako mkali wa jeshi hilo kuweasaka majambazi hayo yanayofanya uhalifu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao kwa mitego ambayo ilitegwa na jeshi hilo katika maeneo tofauti tofauti.
Amesema majambazi hayo kati yao 15 yalikamatwa yakiwa yamevaa mabaibui na madira ili kufanikisha uhalifu wao katika maeneo tofauti ya jiji.
Amesema pia waliweza kukamata bunduki aina ya SMG mopja, Short gun moja, bastola tatu pamoja na risasi kadha walizokutwa nazo wahalifu hao.
No comments:
Post a Comment