
MKE wa Rais Mama Salma Kikwete anusurika kifo kwa ajali mbaya baada ya msafara wake kuingia doa kwa kuvamiwa na lori na kugonga magari matatu ya msafara huo.
Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Rorya mkoani Mara wakati Mama Salma akiwa ziarani mkoani humo.
Kamdanda wea Polisi Tarime, Bw. Constantine Masawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alisema lori hilo lilisimamishwa na askari wa barabarani lisimame ili kupisha msafara huo na kukaidi na kuingia barabarani na kusababisha ajali hiyo.
Amesema kuwa lori hilo liligonga magari matatu ya nyuma ya msafara huo na kusababisha ajali ambayo haikuwa ya lazima wka muda huo.
Amesema lori hilo lilikuwa linaokea nchini Kenya ambapo ilidaiwa pia lori hilo lilikuwa limebeba mali za magendo.
Hivyo imedaiwa dereva huyo ameshikiliwa na jeshi hilo ili kujibu tuhuma hizo.
Hata hivyo hakuna aliyeweza kupoteza masiha kaika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment