Thursday, April 1, 2010
ATUPWA JELA MIEZI 6 KWA KUMUONYESHA MWARABU KIDOLE CHA KATI
Raia wa Uingereza anayeishi Dubai huenda akatupwa jela miezi sita kwa kosa la kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa kiarabu toka Iraq.
Simon Andrews, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 56 anakabiliwa na hukumu ya kwenda jela miezi sita iwapo atapatikana na hatia ya kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa urubani toka Iraq.
Gazeti la The Sun la Uingereza limeripoti kuwa Simon alishindwa kuzizuia hasira zake wakati wa ugomvi wake na mwanafunzi Mahmud Rasheed na kuamua kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati.
Mahmud alikimbilia polisi kupeleka malalamiko yake na haikuchukua muda mrefu Simon alitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mahakamani.
Simon amepigwa marufuku kusafiri nje ya Dubai tangia alipotiwa mbaroni mwezi wa nane mwaka jana.
Akitoa ushahidi wake mahakamani siku ya jumapili, Simon alijitetea kuwa hakufanya kitendo hicho na kwamba raia huyo wa Iraq anamsingizia.
Mahmud hakujitokeza mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Simon na pia hakuna mtu aliyejitokeza kama shahidi wa kesi hiyo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi aprili nne wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment