

Erykah Badu katika video yake iliyosababisha mtafaruku
Mwanamuziki nyota wa Marekani, Erykah Badu ameingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya kuvua zake zote na kubakia uchi katika sehemu ambayo rais wa Marekani, John F Kennedy aliuliwa kwa risasi.
Nyota wa muziki wa R&B, Erykah Badu ameingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya kutengeneza video yake mpya ya muziki akivua nguo na kubakia uchi katika sehemu ambayo rais wa zamani wa Marekani, John F Kennedy alitunguliwa kwa risasi na kuuliwa.
Katika video yake hiyo mpya iliyochukuliwa mjini Dallas bila kibali wala ruhusa ya kujianika hadharani, Badu anaonekana akisaula nguo moja moja hadi kubakia mtupu wa mnyama na kisha kuigiza amepigwa risasi na kuanguka chini akijifanya amefariki.
Rais Kennedy alipigwa risasi na Lee Harvey mwaka 1963 wakati alipokuwa kwenye msafara wa magari ya rais pamoja na mkewe.
Badu ambaye alizaliwa Dallas mwaka 1971 ametoa albamu yake mpya inayoitwa "New Amerykah Part Two: Return of the Ankh".
Badu amesababisha mawazo tofauti toka kwa Wamarekani ambapo wengi wanasema kuwa ameidhalilisha sehemu ya kihistoria kwa kitendo chake hicho ambacho alikifanya mchana kweupe bila ya kujali kama kuna watoto au la.
Taarifa zinasema kuwa polisi huenda wakamkamata na kumtia mbaroni Badu kwa makosa ya kujianika hadharani.
Chini ni VIDEO ya Erykah Badu iliyozua kasheshe.
VIDEO – Nyota wa Marekani Avua Nguo Hadharani
No comments:
Post a Comment