Thursday, April 8, 2010
DIEGO MARADONA ANGATWA USONI NA MBWA WAKE
Diego Maradona aliwahishwa hospitali na kufanyiwa operesheni ya dharura kurekebisha sura yake baada ya kung'atwa vibaya na mbwa wake alipojaribu kumbusu.
Madaktari nchini Argentina walilazimika kumfanyia operesheni ya dharura gwiji wa soka duniani, Diego Maradona ambaye alijeruhiwa vibaya na mmoja wa mbwa wake.
Maradona alishonwa nyuzi 10 kwenye mdomo wake wa juu baada ya kung'atwa na mbwa wake mwenye sura ya kutisha anayeitwa Bela ambaye ni jamii ya mbwa wa kichina wanaoitwa Shar-Pei.
Inadaiwa kuwa Maradona alijaribu kumbusu ili kumliwaza mbwa wake huyo aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo ndipo mbwa huyo kwa hasira alipomshambulia mdomoni.
Maradona alipata majeraha makubwa kwenye mdomo wake wa juu na alikimbizwa hospitali huku akivuja damu nyingi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Maradona atalazimika kupumzika kwa siku tatu baada ya kutumia masaa 15 hospitalini.
Maradona hakuzungumza na waandishi wa habari lakini Fernando Molina, mpenzi wa dada yake Maradona, Dalma, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa Maradona anaendelea vizuri na amepumzika nyumbani kwake.
Maradona aliwahi kulazwa kwenye hospitali hiyo hiyo mwaka 2007 kutokana na maradhi aliyopata kutokana na unywaji pombe uliokithiri.
Maradona mwenye umri wa miaka 49 ndiye anayetarajiwa na Waargentina kuiongoza timu ya taifa ya Argentina kulinyakua kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
Maradona alichaguliwa kuwa kocha wa Argentina mwaka 2008 baada ya kujiuzulu kwa kocha Alfio Basile.
Pamoja na Argentina kutoonyesha uwezo mkubwa katika mechi za hatua ya awali ya kufuzu fainali ya kombe hilo, hatimaye ilifanikiwa kupata tiketi ya kuja Afrika baadae mwaka huu.
Argentina ipo kundi moja na Nigeria pamoja Ugiriki na Korea Kusi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment