Sunday, April 25, 2010
RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA APIMA UKIMWI NA KUWEKA MAJIBU WAPI
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ambaye mwaka 2006 alifanya mapenzi na mwanamke mwenye ukimwi bila ya kutumia kinga na kuzusha uvumi kuwa na yeye ni muathirika, amepima ukimwi na kuweka majibu yake hadharani.
Rais Zuma amewathibitishia watu kuwe yupo fiti na wala hajaathirika kutokana na vipimo vya HIV alivyofanya mwezi huu ambavyo majibu yake yamewekwa hadharani wananchi wayaone.
"Baada ya kuliangalia suala hili kwa umakini nimeamua kuweka wazi majibu yangu ya vipimo vya HIV .. ili kusisitiza uwazi miongoni mwa watu", alisema Zuma.
Rais Zuma alipima 'Ngoma' aprili nne mwaka huu na majibu yalikuwa ni NEGATIVE. Alisema kuwa kabla ya hapo alishafanya vipimo mara tatu na majibu yalikuwa pia NEGATIVE.
Rais Zuma alifanya vipimo hivyo katika kuiunga mkono kampeni ya kuwahimiza watu wapime ukimwi na wazitambulishe hali zao kama wameathirika.
Kampeni hiyo ina malengo ya kuwapima 'ngoma' jumla ya watu milioni 15 ifikapo mwishoni mwa mwezi juni mwakani.
Mwaka 2006, Rais Zuma alifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mwenye ukimwi.
Hata hivyo rais Zuma alikanusha kumbaka mwanamke huyo na kusema kuwa alifanya mapenzi na mwanamke huyo kwa hiari yake mwenyewe.
Rais Zuma alikiri pia wakati huo kuwa alifanya mapenzi na mwanamke huyo bila kutumia kinga ingawa alikuwa akijua fika kuwa mwanamke huyo ni muathirika.
Rais Zuma alisema kuwa siku zote hutumia kondomu lakini siku hiyo alikuwa hana kondomu na mwanamke huyo ndiye aliyeanza uchokozi uliopandisha mashetani yake ya ngono.
Kipindi hicho, Rais Zuma aliamsha hasira za wanaharakati wa kupambana na maambukizi ya ukimwi alipoiambia mahakama kuwa alienda kuoga punde baada ya kumaliza kufanya mapenzi na mwanamke aliyeathirika ili kujiepusha na maambukizi ya gonjwa hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment