Thursday, April 22, 2010
DENI LA TANZANIA LAZIDI KUONGEZEKA
DENI la Taifa limeongezeka maradufu na kufikia shilingi trillion 7.6
Hayo yaliwekwa wazi na katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Otouh, alipokuwa akiwajulisha waandishi wahabari.
Amesema deni la taifa limeongezeka kwa kasi kutoka kiasi cha sh trilioni 6.4 mwaka 2007/08 hadi kufikia shilingi trilioni 7.6 katikka mwaka wa fedha wa 2008/09
.
Amesema kuwa deni hilo limeongezeka kwa tofauti ya shilingi trillion 1.1 kutoka lile la mwaka wa fedha wa jana.
Amesema kutokana na hali hiyo, kuna umuhumu wa serikali kusimamia vizuri makusanyo na matumizi ya fedha zake.
Amesema deni hilo limeongezeka hivyo kutokana na serikali kujiingiza katika bajeti kubwa kuliko uwezo wenyewe.
Vilevile amesema serikali imeshindwa kudhibiti matumizi ya juu, kutokuwa makini na mikataba mbalimbali, pamoja na kuzamini mambo mbalimbali kinyume na uwezo halisi.
Hivyo amesema katika taarifa zilizowasilishwa na maofisa masuuli, zilieleza bayana kuwa wizara, idara, walaka na sekretarieti za mikoa hazikuzingatia kikamilifu sheria ya manunuzi ya umma namba 21 ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005 ambapo jumla ya sh bilioni 12.8 zilionyesha kasoro mbalimbali za ukiukwaji wa taratibu za manunuzi.
Pia alisema katik ukusanyaji wa mapato matokeo ya ukaguzi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), unaonyesha kuwa misamaha mingi iliyotolewa kwa taasisi mbalimbali na watu binafsi yenye thamani ya sh bilioni 752.3 imerudisha nyuma mapato ya serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment