WATU kumi wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kutoka nchini Msumbiji kupinduka katikati ya Mto Ruvuma.
Ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea jana , majira ya saa 7:00 mchana katika Kijiji cha Kiromba Mtwara.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara, Steven Buyuya alisema watu hao walikuwa wakirejea kutoka Msumbiji ambako walikuwa wakitoka katika shughuli zao za kilimo na walipofika eneo hilo upepo mkali uliwakumba na kupoteza mwelekeo na mtumbwi huo ukazama majini.
Kamanda alisema mtumbwi huo ulikuwa umebeba abiria 12 na walionusurika ni nahodha na abiria mmoja ambao ni Idrisa Nkerewe aliyekuwa nahodha na Abdallah Kaisi, 32 abiria
Alisema kuwa tayari miili ya watu watatu imeshapatikana na majina na maeneo wanapoishi yametambulika.
Friday, April 16, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment