MAHAKAMA YA RUFAA ya Tanzania jana ilitengeua na kuondoa suala la mgombea binafsi na haitatumika katika uchaguzi tarajio kwa kuwa suala hilo limeonekana kuwa ni la kisiasa zaidi na si la kisheria.
Uamuzi huo uliotolewa jana na jopo la majaji saba na kusomwa na Jaji Mkuu, Agustino Ramadhani, na kusema mgombea binafsi hataruhusiwa katika uchaguzi ujao wa Oktoba mwaka huu.
Akisoma hukumu hiyo, katika ukumbi wa mahakama kuu, Jaji Ramadhani alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa mahakamani, mahakama imegundua kuwa suala la mgombea binafsi ni la kisiasa, hivyo mahakama haina mamlaka ya kulitolea uamuzi.
Alisema uamuzi wa kuwa na mgombea binafsi ni suala la kisiasa linapaswa kuzingatia historia na matakwa ya nchi husika, hivyo mahakama imependekeza suala hilo lirudishwe bungeni ili lijadiliwe kwa kina zaidi na kutolewa uamuzi huko kwa kuwa bunge ndicho chombo kitachokuwa na mamlaka ya kufanya mabadiriko ya katiba za nchi
“Kwa mujibu wa ibara ya 98 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bunge ndilo lenye jukumu la kufanya marekebisho ya vipengele vya katiba au sheria yeyote”
Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakamani hapo mmoja wa wadai wa ugombea binafsi, Mchungaji Chisptopher Mtikila alipohojiwa na vyombo vya habari kuhusiana na hukumu hiyo alisema, hakustushwa sana na maamuzi ya jopo hilo la majaji kwa kuwa tayari alikwishaanza kuona dalili ya mahakama kumpendelea Rais Jakaya Kikwete ili arudi madarakani.
Alisema ka kuwa hakuridhika na maamuzi hayo, anakusudia kuwasilisha rufaa mbele ya Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki ili litolewe uamuzi ambao anaamini utakuwa wa haki.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi waliohudhuria hukumu hiyo wanasheria na wanaharakati mbalimbali walionekana dhahiri kusikitishwa na maamuzi hayo na kusema kuwa mahakama hiyo haijali maslahi ya wananchi na wanyonge wan chi hii.
Walisema maamuzi hayo wamepokea kwa masikitiko makubwa za kusitisha mgombea binafsi na kusema kuwa mahakama imeshindwa kushughulikia mambo ya msingi yalnayohitaji majibu kutoka kwenye chombo hicho na wameona maamuzi hayo ni kama kutowatendea haki wananchi.
No comments:
Post a Comment