Mwanaume mmoja wa nchini Marekani anakabiliwa na kifungo cha miezi 108 jela baada ya kukiri kulichoma moto kanisa la watu weusi ili kupinga Barack Obama kuwa rais mweusi wa Marekani.
Benjamin Haskell, 23, wa Massachusetts nchini Marekani amekiri kosa lake la kulichoma moto kanisa la Wamarekani weusi ili kupinga kuchaguliwa kwa Barack Obama kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani.
Benjamin alikiri jana kulichoma moto kanisa la Macedonia Church of God in Christ mnamo novemba 5 mwaka 2008, ikiwa ni ndani ya masaa machache baada ya Obama kuchaguliwa kuwa rais.
Benjamin alilimwagia petroli kanisa hilo kabla ya kulipiga kiberiti na kuliteketeza.
"Leo tunatoa ujumbe kuwa watu wanaofanya uhalifu kwa sababu za chuki, watachunguzwa na baadae ya kushtakiwa", alisema Carmen Ortiz mwanasheria mkuu wa Massachusetts.
Benjamin huenda akahukumiwa kwenda jela miezi 108 (miaka 9) baada ya kukiri kosa lake la kuhatarisha maisha ya waumini 300 wa kanisa hilo na kuliharibu jengo la kidini kwasababu ya chuki zake ubaguzi wa rangi.
No comments:
Post a Comment