MADEREVA na makondakta wa daladala wa jijini Dar es Salaam wametangaza mgomo wa kuacha huduma hiyo ambayo walidai utaanza leo.
Mgomo huo tarajio ulisambazwa kwa njia ya vipeperushi na baadhi ya madereva wa jijini humo na mgomo huo utahusisha njia zote za mkoa wa Dar es Salaam.
Sababu ya kuanzisha mgomo huo ulidaiwa na maderava hao kuwa ni maslahi duni kwa siku, na kubwa ni kero za barabarani zinazosababishwa na Kampuni ya Majembe na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani (Trafiki) ambao wamekuwa wakiwasumbua kila siku kwa sababu ambazo hazina msingi.
Madai mengine ni kutaka kuwekewa mazingira bora ya kazi ikiwemo mishahara, na makato ya mishahara hiyo ipelekwe Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa lengo ya kuboresha kazi hiyo kama wafanyakazi wengine nchini.
No comments:
Post a Comment