Monday, March 29, 2010
MWANAME MWENYE MATITI MAKUBWA DUNIANI TOKA CHINA
Guo Feng mwanaume mwenye matiti makubwa Monday, March 29, 2010 4:58 AM
Madaktari nchini China wanadai kumgundua mwanaume mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani.
Madaktari nchini China wanadai kumgundua mwanaume mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani baada ya mwanaume huyo kujitokeza kwenye kliniki moja mjini Beijing.
Daktari wa hospitali ya Jinan Chest Hospital, Dokta Zhang Lilan alisema "Huyu ni mwanaume kamili isipokuwa ana matiti kama mwanamke".
"Yeye ni mkulima na anasema kuwa anasumbuliwa na ukubwa wa matiti yake wakati anapofanya kazi zake za kilimo".
"Anasema pia matiti yake yamekuwa gumzo kijijini kwake ambapo watu wengi wamekuwa wakimtafuta ili kumuona na imekuwa kero kubwa sana kwake kiasi cha kumfanya awe anavaa makoti makubwa hata wakati wa joto kali ili kuyaficha matiti yake", alisema dokta Lilan.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Guo Feng mwenye umri wa miaka 53, alisema "Miaka 10 iliyopita matiti yangu yalianza kuwa makubwa lakini nilikuwa nikifikiria unene wangu ndio sababu .. lakini miaka michache iliyopita nimekuwa nikizunguka hospitali moja baada ya nyingine kutafuta tiba lakini hakuna mtu anayetaka kunisaidia".
"Nimetumia pesa nyingi sana kwenye vipimo hospitalini lakini hakuna jibu lolote la maana huku matiti yangu yakiendelea kuwa makubwa", alisema Guo Feng.
"Wakati mwingine huwa nafikiria madaktari hawataki kunisaidia", alilamika Guo Feng.
Dokta Lilan alisema kuwa Guo Feng ametishia kuyakata matiti yake yeye mwenyewe iwapo hakuna daktari atakayejitokeza kumpatia tiba.
Hata hivyo madaktari wamekataa kuchukua hatua yoyote mpaka watakapogundua sababu ya matiti yake kuwa na ukubwa huo usio wa kawaida.
"Katika miaka yangu 30 ya kufanya kazi ya udaktari sijawahi kukumbana na kitu kama hichi", alisema Dokta Lilan.
"Awali tulidhania amekula kitu chenye sumu lakini vipimo vya damu yake havijaonyesha kitu chochote. Tumemfanyia X-ray hana dalili ya kansa", aliongeza mmiliki wa hospitali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment