Monday, March 29, 2010
MTOTO MWENYE VIDOLE 31 TOKA CHINA
Mtoto huyu wa nchini hana idadi ya vidole vya miguu na mikono kama watu wengine, amechukua rekodi ya dunia kwa kuwa na jumla ya vidole 31.
Mtoto mwenye umri wa miaka sita wa nchini China analazimika kufanyiwa operesheni ili kupunguza idadi ya vidole vyake vya mikono na miguu.
Mtoto huyo wa mji wa Shenyang katika jimbo la Liaoning kaskazini mwa China ana jumla ya vidole 16 vya miguu na vidole 15 vya mikono.
Vidole vyake vitatu katika kila mkono wake vimeungana pamoja.
Idadi ya vidole vyake inavunja rekodi ya dunia ya vidole 25 iliyokuwa ikishikiliwa na watoto wawili wa India Pranamya Menaria na Devendra Harne, ambao kila mmoja wao ana vidole 12 vya mikono na vidole 13 vya miguu.
Hata hivyo mtoto huyo wa nchini China atafanyiwa operesheni ya kupunguza idadi ya vidole vyake wiki hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment