
JESHI la Polisi Nchini, limetoa kitabu maalum kinachofafanua na kumuongoza mwananchi mchakato mzima wa uchaguzi kwa lengo la kuwezesha uchaguzi, huo kufanyika kwa utulivu na amani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema alisema kitabu cha Haki na wajibu wa Mpigakura, kimebeba ujumbe mzito unaohusu kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mwema alisema ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza vigezo wa kupiga kura kitabu hicho kitamuongoza katika kuhakikisha kuwa sheria za nchi hazikiukwi kabla na baada ya uchaguzi
Alisema kitabu hicho kinalenga kuufanya uchaguzi huo uwe wa haki katika kuchagua viongozi na kutekeleza wajibu wa usalama, amani na utulivu vinadumu katika jamii.
Alisema kitabu hicho kinaelezea umuhimu wa kujiandikisha kupiga kura, uteuzi wa wagombea katika vyama vya siasa, kampeni za wagombea na vyama vyao na matangazo yatakayowekwa na vyama vya siasa na wagombea.
Mambo mengine ni wajibu na umuhimu wa polisi katika mchakato wa uchaguzi, haki na wajibu wa mpigakura, siku ya uchaguzi, jinsi ya kupiga kura, kusubiri matokeo, kupokea matokeo na uvunjaji wa sheria wakati wa uchaguzi.
Pia alisema “askari polisi watakaovujisha siri za taarifa mbalimbali zinazohusu mitaa katika uchaguzi watachukuliwa hatua kali, pia na mwananchi yeyote atakayehatarisha hatari ama kugundulika kuvunja amani sheria itafata mkondo wake” alisema.
No comments:
Post a Comment