Monday, April 19, 2010
APIGIWA KURA YA U MEAYA WAKATI WAMESHA FARIKI
Wapiga kura nchini Marekani wamemchagua mtu aliyefariki awe meya wao mpya.
Carl Geary alifariki mwezi mmoja uliopita kutokana na shambulio la moyo wakati akipiga kampeni za kuwania umeya wa mji mdogo wa Tracy City, Tennessee nchini Marekani.
Lakini pamoja na kwamba watu wengi walikuwa wakijua kuwa ameishafariki, marehemu Carl alishinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi sana mara tatu zaidi ya mpinzani wake.
Mjane wa marehemu Bi Susan Geary alisema kuwa matokeo ya uchaguzi hayamjashangaza kwani aliyatarajia.
"Siku aliyofariki watu walikuwa wakinipigia simu kutoa salamu za rambirambi wakisema kuwa watampigia kura kwenye uchaguzi".
Carl aliyefariki akiwa na umri wa miaka 55, alijulikana sana kwa misimamo yake thabiti ya kisiasa.
Pamoja na kwamba alishazikwa wiki kadhaa zilizopita, Carl alishinda uchaguzi kwa kupata kura 285 huku mpinzani wake akiambulia kura 85.
Mmoja wa wafanyabiashara katika mji huo alisema kuwa watu waliamua kumpigia kura Carl ili kuonyesha upinzani wao kwa meya aliyopo madarakani Bi. Barbara Brock.
"Nilikuwa nikijua kuwa ameishafariki, najua watu wataona kama ni upuuzi lakini tulitaka tupate meya mwingine sio huyu aliyepo", alisema Chris Rogers, mmiliki wa mgahawa mmoja uliopo mjini humo.
"Kama uchaguzi utarudiwa tena wiki ijayo nitampa kura yangu tena marehemu".
Maafisa wa mji huo wamesema kuwa manispaa itafanya kikao kuamua nani awe meya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment