Monday, April 12, 2010
KIKWETE KUFUNGUA SEMINA YA UKIMWI KWA WANAJESHI
RAIS Jakaya Kikwete kesho anatarajia kufungua kongamano la kimataifa kuhusu tatizo la ugonjwa ukimwi katika majeshi litakalofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC mjini hapa.
Kongamano hilo, linatarajia kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 260 kutoka nchi 70 ambapo hadi sasa nchi 60 zimethibitisha kushiriki kongamano hilo ambalo linaelezwa kuwa la kwanza kufanya nchini.
Msemaji wa jeshi hilo, Luteni Kanali Kapambala Mgawe, alisema kongamano hilo litahudhuriwa na makamanda kutoka nchi za bara la Afrika, Asia, Amerika, Carribean, Ulaya na Marekani.
Luteni Kanali Mgawe, alisema mbali na makamanda wa jeshi pia taasisi za kimataifa zinazojihusisha na mapambano dhidi ya ugonjwa huo zitahudhuria.
Kongamano linafanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na jeshi la Marekani kuhusu masuala ya ukimwi kutokana na askari wengi kufariki kwa ugonjwa huo.
Alisema pia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania, Jenerali Aden Mwamunyange, pamoja na makamanda wa ngazi ya juu kutoka JWTZ watahudhuria.
Alisema kongamano hilo linafanyika kwa ushirikiano wa pamoja kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Wizara ya Ulinzi ya Marekani kwa lengo la kukabiliana na tatizo la ugonjwa ukimwi ndani majeshi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment