
JANA jiji la Dar es salaam lilitawaliwa na shida na mapungungufu makubwa katika huduma mbalimbali kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku nzima hali iliyofanya wakazi wa jiji kuteseka kutokana na hali hiyo.
Mbali na kuwa na dmapungufu katika huduma nyingine tofautitofauti shida kubwa zaidi ilikuwa ni upande wa usafiri ambao ulikuwa haupatikani kutokana na mvua hiyo.
NIFAHAMISHE ilishuhudia makundi ya watu yakihaha huku na huku, na yakipita barabarani mithili ya maandamano yakitembea kwa miguuu kurudi majumbani mwao kwa kukoseskana kwea huduma hiyo.
Hali hiyo ilidumu siku nzima katika kila kituo cha mabasi jijini ambapo mabasi yalikuwa hayafiki mjini na wakazi hao kulazimika kurudi kwa miguu majumbani mwao.
Jopo la waandishsi wa nifahamishe nao dhahama hiyo iliwakumba kwa kile kilichowakuta wamefika kituoni Posta majira ya saa 11 ya jioni na hadi ilipofika majira ya saa moja kasorobo hawajapata usafiri na kulazimika watembee kwa miguu kuhamia katika kituo cha nyuma cha Akiba na hali ilikuwa hivyohivyo.
Hali ilivyozidi kuwa tata zaidi waliamua warudi nyuma na kuelekea kituo cha fire ili waweze kupata usafiri na wageuze na mabasi lakini hali hiyo walidumu nayo kwa takribani dakika 45 kituoni hapo bila kuwa na dalili yoyote ya kupata usafiri.
Hiyo ndiyo hali iliyokuwa jana katika jiji la Dar es Salaam kwa wakazi wengi waishio humo wakionekana kurudi kwa miguu kutokana na adha iliyokuwepo
No comments:
Post a Comment