WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Wednesday, April 28, 2010

OBAMA NA AGA KHAN WAGUSWA NA MUUNGANO TANZANIA



RAIS Barack Obama wa Marekani na Aga Khan Kiongozi wa wa Ismailia duniani wamemtumia Rais Jakaya Kikwete salamu za pongezi kwa kwa kusherehekea sikukuu ya Muungano iliyoadhimishwa jana nchini kote.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana ikinukuu taarifa ya ubalozi wa Marekani hapa nchini ilielezea kuwa salamu hizo kutoka kwa viongozi hao zilitumwa jana.

“Mpendwa Rais, kwa niaba ya watu wa Marekani, nakutumia salamu zangu za dhati kukupongeza wewe na watu wa Tanzania, wakati mnaposherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26, April,” ilieleza sehemu hiyo ya taarifa iliyopitia Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

“Ni matumaini yangu kwamba miaka ijayo italetea Watu wa Tanzania Amani na mafanikio ya kudumu,” Rais Obama alimueleza Rais Kikwete katika salamu hizo na kuelezea nia yake na matarajio ya baadaye kuwa nchi hizo zitaimarisha mahusiano baina yao.

“Natarajia tutaimarisha na kuwa na mahusiano thabiti baina ya nchi zetu,” salamu za Rais Obama ilieleza.

Naye Kiongozi wa wa Ismailia duniani alimueleza Rais Kikwete furaha yake na kutoa salamu za heri kwa Rais Kikwete na Watanzania wote.

“Wa-Ismailia Imamat na Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, kwa pamoja tunaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania na Jumuiya za Kiraia katika kuchangia katika ukuaji wa nchi na nafasi kwa watu wote wa Taifa,” alieleza na kumshukuru Rais Kikwete kwa ushirikiano wake.

“Tunathamini ushirikiano wako na wa Serikali yako katika kuunga mkono na kutia moyo shughuli za Jumuiya ya Aga Khan,” Salamu za Aga Khan zilielezea.

Jana maelfu ya watu walioenda kushuhudia sherehe za maadhimisho ya Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walionyesha hisia zao wakati marais wastaafu, Ali Hassani Mwinyi na Benjamini Mkapa walipoingia.

Umati huo ulilipuka shangwe za kelele na vifijo wakati viongozi hao walipoingia kwenye uwanja huo mkongwe kwa nyakati tofauti kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuingia na kuzunguka uwanja mzima akipunga mkono.

Mkapa, ambaye aliongoza serikali ya awamu ya tatu ambayo ilijipatia sifa ya kuinua uchumi na kuboresha miundombinu, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia uwanjani katika siku hiyo iliyokuwa na jua la vipindi.

Baada ya Mkapa, ambaye aliongoza nchi kwa sera aliyoiita ya "ukweli na uwazi", kuingia uwanjani hapo kwa gari la kifahari aina ya Range Rover (Vogue), kelela za shangwe na vigelegele zililipuka kutoka kwenye umati wa watu.

Mkapa aliyeingia uwanjani hapo majira ya saa 3:15 alipishana kwa takriban dakika 15 na kiongozi wa serikali ya awamu ya pili, Mwinyi ambaye pia aliamsha kelele za shangwe kutoka kwa watu waliohudhuria.

Kama ilivyokuwa kwa Mkapa, Mwinyi ambaye aliingia uwanjani hapo na gari aina ya Toyota Landcruiser (VX) alishangiliwa kwa nguvu tofauti na ilivyokuwa kwa viongozi wa serikali ya sasa, akiwemo Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment