
Mwanamke wa nchini Uingereza aliyesherehekea kutimiza umri wa miaka 34 kwa kutoboa ulimi wake kuweka kichuma amefariki siku mbili baadae kutokana na sumu iliyotokana na kichuma hicho.
Amanda Taylor alipuuza kauli za familia yake kumpinga kuweka kichuma cha inchi moja kwenye ulimi wake na aliamua kuutoboa ulimi wake kuweka kichuma hicho ili kusherehekea kutimiza umri wa miaka 34.
"Kwa muda mrefu alifikiria kuutoboa ulimi wake kuweka kichuma", alisema mama yake Lorraine Taylor mwenye umri wa miaka 61.
"Siku nne kabla ya siku yake ya kuzaliwa aliniambia kuwa anataka kuweka kichuma kwenye ulimi wake siku ya kuzaliwa kwake", aliendelea kusema mama yake.
"Nilimpinga na kumuonya asifanye hivyo lakini alisema kuwa marafiki zake wote wameishaweka vichuma kwenye ndimi zao".
Kwa shingo upande mama yake alimpa ruhusa Amanda kutoboa ulimi wake lakini siku mbili baadae Amanda alikutwa nyumbani kwake akiwa amefariki.
Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa alifariki kutokana na damu yake kuingia sumu iliyotokana na kichuma alichowekewa kwenye ulimi wake.
Uchunguzi zaidi kuhusiana na kifo chake unaendelea.
No comments:
Post a Comment