Friday, March 26, 2010
AJALI MBAYA DAR, HIACE YAKANDAMIZWA NA LORI
ZAIDI ya watu nane wamepoteza maisha papohapo kwa ajali mbaya iliyotokea huko maeneo ya Kibamba Darajani nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Ajali hiyo ilitokea jana, majira ya saa 11 alfajiri ambapo ilihusisha gari aina ya lori lililokuwa na namba za usajili T 189 na basi dogo la abiria aina Toyota Hiace lililokuwa na namba za usajili T 616 AJW.
Ajali hiyo imetokea baada ya lori hilo lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Pwani kupoteza mwelekeo na kuingia kulia zaidi na kuivaa basi hilo uso kwa uso lililokuwa na abiria na kulilalia na kupoteza maisha ya watu hao.
Hiace hiyo ilikuwa inatoka Lugoba mkoani Pwani ilikuwa inaelekea Dar es Salaam na ndipo ilipovamiwa na lori hilo na abiria wote waliokuwemo humo kufariki dunia papohapo na kati yao kulikuwa na mamda mjamzito.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa lori hilo lilikuwa imeshindwa kuhimili breki na kudaiwa halikuwa na breki na ndicho chanzo kikuu cha ajali hiyo mbaya.
Hata hivyo mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo dereva wa lori na utingo wake wlikimbia na kuacha lori hilo papohapo na hawakujulikana mara moja walikimbilia wapi kwa muda huo.
Katika hali ya kushangaza wananchi bado hawajifunzi na baadhi ya maelfu waliokimbilia katika ajali hiyo kuonekana kuzoa mafuta ya taa yaliyomwagika barabarani na kusahau kuwa siku za karibuni watu walipoteza maisha kutokana na matukio kama hayo walikuw wnazoa mafuta na ghafla lori kulipuka na kupoteza maisha na wengine walipata vilema vya maisha kutokana na
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment