Friday, March 26, 2010
NYUKI WENYE HASIRA WAUA MIFUGO NA KUJERUHI WATU 40
Nyuki wenye hasira walikitesa kijiji kizima nchini Niger kwa masaa kadhaa na kuua mifugo kadhaa pamoja na kuwafanya watu zaidi ya 40 wakimbizwe hospitali wakiwa majeruhi. Kundi la nyuki waliokuwa na hasira baada ya mzinga wao kwenye mti kung'olewa, walikitesa kijiji kimoja kusini mwa nchi ya Niger kwa kuwashambulia watu na mifugo kwa masaa kadhaa.
Watu zaidi ya 40 wakiwemo watoto 14 waliwahishwa hospitali baada ya kushambuliwa na nyuki wakati mzinga wa nyuki uliokuwa kwenye mti mkubwa kwa zaidi ya miaka 50 ulipodondoshwa chini kutokana na upepo mkali.
Punda mmoja na farasi mmoja walifariki dunia huku ng'ombe na mbuzi 95 wakiachwa wakiwa wamepooza miili yao baada ya kudungwa sindano za nyuki hao wenye hasira.
Kwa mujibu wa radio Anfani ya nchini Niger, nyuki walikivamia kijiji cha Dake-Garka katika mji wa Birni-N'Konni baada ya tawi la mti lililokuwa na mzinga wao, lilipoangushwa chini na upepo mkali.
Iliripotiwa kuwa masaa kadhaa baada ya uvamizi wa nyuki hao, wanakijiji walikuwa bado wanahofia kurudi kwenye majumba yao kwa kuhofia mashambulizi ya nyuki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment