Friday, March 26, 2010
APOTEZA MAISHA KWA MOTO KISA KUKATALIWA
Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye alitoswa na mkewe wa ndoa ya miaka 14 ambaye alipata mwanaume mwingine nje, amefariki dunia kutokana na moto aliouanzisha ili kuichoma moto nyumba yake ili mkewe asiambulie kitu watakapoachana. Wakati Timothy Flood alipoimiminia petroli nyumba yake ili ndoa yake na mkewe itakapovunjika, mkewe asiambulie kitu, hakungundua kuwa kuna kiasi kidogo cha petroli kilimwagikia kwenye nguo zake.
Na wakati alipoipiga kiberiti nyumba yake alishangaa kujikuta na yeye mwenyewe akiwaka moto.
Timothy ambaye ni baba wa watoto watatu alijaribu kuuzima moto uliokuwa ukimteketeza kwa kutumia maji ya mvua lakini hadi wakati anaokolewa alikuwa ameishangua asilimia 90 ya mwili wake na alifariki dunia siku mbili baadae hospitalini.
Timothy mwenye umri wa miaka 42, aliamua kuichoma moto nyumba yake baada ya mkewe kuamua kuivunja ndoa yao alipoanza uhusiano na mwanaume aliyesoma naye shule.
Ingawa Timothy na mkewe, Catherine, 39, walikuwa wakiendelea kuishi kwenye nyumba moja walikuwa hawazungumzi wala kujuliana hali.
Mgogoro mkubwa ulikuwa kwenye nyumba yao ambapo Catherine alimtaka Timothy aondoke amuachie yeye nyumba hiyo.
Timothy kwa kuhofia kuwa watakapoachana rasmi kisheria kutokana na sheria mkewe anaweza akapewa nyumba kwa sababu ya watoto wao,
aliamua kuichoma moto ili wakose wote.
Mahakama katika mji wa Newport, kusini mwa Wales iliambiwa kuwa Timothy ili kuichoma moto nyumba hiyo alinunua lita 51 za petroli na viberiti kadhaa ili kuhakikisha kuwa hakitoki kitu.
Siku ya tukio, alimpeleka mkewe kwa wazazi wake na ndipo aliporudi na kuipiga moto nyumba hiyo baada ya kumtumia meseji mkewe akimwambia "Nimeishapata suluhisho la kuishi bila wewe".
Moto mkubwa ulizuka ambao uliiteketeza sehemu kubwa ya nyumba hiyo.
Majirani wanasema kuwa Timothy alisikika akipiga kelele za kuomba msaada wakati moto aliouanzisha akitegemea kuiteketeza nyumba yake ulipokuwa ukimchoma yeye mwenyewe.
Timothy alifariki siku mbili baadae hospitalini baada ya ndugu zake kukubali kuzizima mashine zilizokuwa zikimsaidia aendelee kuishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment