MAHABUSU watano jana walitoa kioja cha mwaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni walijipaka kinyesi kwa kugoma kurudi mahabusu. Washitakiwa hao wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa kutumia silaha wote kwa pamoja walichukua uamuzi huo baada ya kugoma kurudi mahabusu kwa kutaka wafutiwe mashitaka yao ambayo yamedumu wka muda mrefu.
Hivyo washitakiwa hao walipotakiwa na askari magereza kutoka mahabusu na kuelekea mahakamani walichukua vinyesi na kujipaka mwilini.
Hali ilikuwa tata walipofika mahakamani hapo hali iliyoradhimu hakimu kushindwa kuendelea kusikiliza shauri hilo kwa siku hiyo.
Mahabusu hao walionekana kugoma kupanda basi maalum linalowarudisha rumande kwa madai ya kutaka kufutiwa shauri hilo hali iliyofanya wapakiwe kwenye gari dogo na kupelekwa kituo cha polisi Magomeni.
Friday, March 26, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment