Mwanaume mmoja nchini Urusi anashikiliwa na polisi baada ya kuanzisha mchezo wa kuchezea bunduki katikati ya sherehe za harusi na kupelekea mwanaume mmoja ajipige risasi ya kichwa. Huku bwana harusi na bi harusi wakiangalia kwa mshtuko mkubwa, mwanaume aliyepewa bunduki aigize anajipiga kichwani baada ya kuambiwa kuwa bunduki hiyo haina risasi, aliichukua bunduki na kuielekeza kichwani mwake.
Huku watu wengine wakimsihi asijaribu kufanya hivyo, mwanaume huyo aliielekeza bunduki kichwani na alipoifyatua risasi ilitoka kweli na kulifumua fuvu la kichwa chake.
Mwanaume huyo amelazwa hospitali akiwa amepooza mwili wake huku ubongo wake ukiwa umeharibiwa vibaya na risasi hiyo.
Kasheshe hilo lilianza kwa mwanaume mmoja ambaye ni rafiki wa bwana harusi alipotoa bunduki na kuwaalika watu waje kucheza mchezo unaoitwa "Russian Roulette".
Mwanaume huyo alijielekezea mwenyewe risasi na kuifyatua lakini risasi haikutoka. Ndipo alipomualika mtu mwingine naye aje ajaribu.
Video ya tukio hilo iliyowekwa kwenye tovuti ya YouTube inamuonyesha mwanaume huyo akiichukua bunduki na kuielekeza kichwani kwake kabla ya kuifyatua na yeye mwenyewe kuanguka chini na kuzua mshikeshike kwenye harusi hiyo.
Rafiki huyo wa bwana harusi anashikiliwa na polisi ingawa alijitetea kuwa alikuwa akijua kuwa bunduki yake ilikuwa tupu haina risasi.
Mchezo wa Russian Roulette ulikuwa ukifanyika kwenye jela za Urusi wakati wa miaka ya mapinduzi ya Urusi ambapo wafungwa walilazimishwa kuzichezea bunduki huku maafisa wa jela wakicheza kamari kujua mfungwa yupi atafariki kwanza.
Chini ni VIDEO ya tukio hilo la kwenye harusi.
No comments:
Post a Comment