WASICHANA wawili wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu baada ya kuchaniwa nguo zao walizovaa kwa kuonekana walikuwa wabishi baada ya kukutwa na askari wa mtaani maarufu kama sungusungu.
Wasichana hao majina hayakuweza kupatikana mara moja walikutwa na dhahama hiyo, juzi majira ya usiku huko maeneo ya Mnazi Mmmoja jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari hao jamii wanaoshirikiana a askari wa jeshi la polisi walidai waliwakuta wasichana hao wamevaa nusu uchi na kuwasimamisha kwa kuwa wao walikuwa lindo kusaka waharifu wapitao majira hayo.
Walidai kuwa walipotakiwa kusimama walionekana kukaidi na kutaka kuondoka bila kutambua watu hao walikuwa katika lindo.
Hivyo walipoonekana kubisha zaidi wanalindo hao waliwabeba kwa nguvu na ndipo nguo zao zilipochanikia kwa kuwa walikuwa wakaidi kwenda kituoni cha polisi kwa mahojiano.
Mmoja wa askari hao aliokuwa eneo la tukio alidai wasichana hao baada ya kutakiwa kwenda kituo cha polisi walifungua mikoba yao na kutoa magauni marefu kutak kuvaa maarufu kama Madera na kuzuiliwa wafike hivyo hivyo kituoni.
JEshi la polisi wameunda vikosi maalum vya mitaani vya ulinzi vinavyojulikana polisi jamii ewanaoshirikana na askari kukamata waharifu mitaani.
Thursday, March 25, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment