MWANAMKE Sophia Philemon [44] ambaye ni mama wa watoto watatu, amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi chini ya miaka 18. Mwanamke huyo mkazi wa wilayani Moshi vijijini alifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Langasani mwenye umri wa miaka 15 bila kutambua anatenda kosa kisheria.
Hukumu hiyo takatifu, ilitolewa jana na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi John Nkwabi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, John Nkwabi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.
Nkwabi alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa akiwemo na mwanafunzi huyo umeithibitishia mahakama pasipo shaka yoyote na mahakama imeridhika na ushahidi huo.
Nkwabi alisema kitendo alichokifanya mwanamke huyo cha kumlazimisha kijana huyo kufanya nae tendo la ndoa ni kosa chini ya kifungu namba 138B (1) (d) cha kanuni ya adhabu kinachosimamia makosa ya kimapenzi kwa watoto baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali hati ya mashitaka ilionyesha kuwa, Februari 28, mwaka jana, saa 1:00 usiku, huko katika kambi namba tisa katika nyumba za sukari wilayani Moshi vijijini, mshitakiwa alimlazimisha mwanafunzi huyo kufanya naye mapenzi katika chumba anachoishi na mumewe.
Ilidaiwa kuwa muda huo mwanafunzi huyo alikuwa ametoka dukani alikokuwa ametumwa na wazazi wake na mwanamke huyo alimwita na kumshawishi aingie ndani ya nyumba yake anapoishi na mumewe na baadaye kumlazimisha kufanya naye tendo la ndoa.
Sophia ni mke wa mtu na ni mama wa watoto watatu ambao wawili wa kike na mmoja ni wa kiume.
Thursday, March 25, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment