MWANAMKE mmoja jana aliingia matatani baada ya kushindwa kuvumilia matusi aliyokuwa akitukanwa na mgonjwa wa kifua kikuu na kujikuta akimpiga ili aweze kumliza hasira zake. Tukio hilo lilitokea jana majira ya jioni, huko Mbagala Charambe baada ya mwanamke huyo [jina kapuni] kumpa kipigo mgonjwa huyo ambaye anaumwa kwa muda mrefu.
Ilidaiwa mwanamke huyo ambaye anaishi jirani na anakoishi mgonjwa huyo, alipatwa na jazba baada ya mgonjwa huyo kumtukana matusi na kushindwa kuvumilia na kumtia mikononi.
Ilidaiwa mgonjwa huyo alimtukana mama huyo matusi ya nguoni na ilidaiwa ni kawaida yake kumtuakana masma huyo na siku hiyo alishindwa kuvumilia na kumtiq mikononi.
Ilidaiwa ndugu wa mwanamke huyo walimsihi asimpige mgonjwa huyo japo kuwa anamatatizo mana alikuwa anatumia kigezo cha ugonjwa wake na kumsihi anaweza akapatwa na matatizo..
Bila kutambua alijikuta akimuingia mgonjwa huyo na ndugu wa mgonjwa huyo kuchachamaa na kwenda kuripoti kituo cha polisi.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alitakiwa kituo cha polisi akatoe maelezo machache kuhusiana na sakata hilo.
Kitakachoendelea kitawajia baada ya kupata tarifa kamili
YAKUSANYA TRILIONI 7.53 JANUARI HADI MACHI 2025
3 minutes ago
No comments:
Post a Comment