WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Thursday, March 25, 2010

MITI 6OOO YAKATWA KUZUIA WATU KUFANYA MAPENZI UKO UINGEREZA




Miti ipatayo 6,000 iliyopo pembeni mwa barabara moja kuu nchini Uingereza imekatwa ili kuwazuia watu kupeana huduma za chap chap. Miti zaidi ya 6,000 iliyopo pembeni barabara namba A666 katika mji wa Darwen kaskazini masharibi mwa Uingereza imeteketezwa ili kuwazuia watu kufanya mapenzi chini ya miti hiyo.

Miti hiyo iliyochukua eneo la hekta 12 ilikuwa ni maarufu kama kituo cha watu wanaopeana huduma za mapenzi za chap chap.

Miti hiyo iliyopandwa baada ya vita vya pili vya dunia, ilikatwa baada ya maafisa wa manispaa ya mji huo kudai kuwa miti hiyo imezeeka na inaweza ikayaangukia magari yanayopita kwenye barabara hiyo.

Lakini sajenti wa polisi Mark Wilson alisema kuwa miti hiyo ilikatwa kutokana na kuwa kero kwa wapitanjia kutokana na baadhi ya watu kupenda kufanya mapenzi kwenye maeneo ya miti hiyo huku wakionekana wazi.

"Lilikuwa ni tatizo la muda mrefu lililoleta kero kero kubwa sana kwa jamii", alisema sajenti Wilson.

Haijajulikana kama kukatwa kwa miti hiyo kutaleta ufumbuzi wa tatizo hilo la watu kujisevia pembeni mwa barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment