WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Thursday, April 8, 2010

ZITTO KABWE:WANA SIASA WALAUMIWE KUUZWA KWA MITAMBO


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amesema wanasiasa nchini ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa hatua ya kuuzwa nje, mitambo ya kufulia umeme wa gesi ya Dowans Tanzania.

Kauli ya Zitto imekuja baada ya serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kushindwa kununua mitambo hiyo baada ya maombi yao kupingwa na wanasiasa.

Zitto alitoa shutuma hizo juzi jijini Dar es Salaam katika ofisi ndogo za Bunge, alipokuwa akizungumza kikao cha kujadili ripoti ya hesabu za Tanesco za mwaka 2008.

Ripoti hiyo ilikuwa imewasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu ya Mashirika ya Umma(POAC).

Taarifa ya kuuzwa kwa Dowans ilibainishwa na Zitto katika kikao hicho.Hata hivyo Zitto hakutaja kampuni iliyonunua mitambo hiyo, wala nchi ilipouzwa, au gharama zake.

"Tayari mitambo ya Dowans imekwishauzwa nje ya nchi. Katika hili wanaotakiwa kulaumiwa ni sisi wanasiasa na si vinginevyo kwa kuwa walipinga Tanesco kununua mitambo hii," alisema Zitto

Hata hivyo mwanasheria wa Tanesco, Subira Wandiba alisema mitambo ya Dowans ya megawati 112 imezwa kwa Tanesco kupitia mahakama, kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni hiyo iliyorithi mkataba tata wa Richmond Dvelopment LLC.

Alisema hatua hiyo imefanyika kwa matarajio kuwa kama itashinda kesi hiyo, mitambo hiyo itatumika kama fidia.

Februari 21, 2009 Tanesco iliwasilisha dhamira yake ya kutaka kununua mitambo ya Dowans na ilitoa sababu za kiuchumi na kimahitaji za kutetea uamuzi wake huo.

Hatua ya ilikuja takriban miezi miwili tangu uamuzi wake huo ukataliwe katakata na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini Desemba mwaka 2008.

Pamoja na mambo mengine, Tanesco chini ya aliyekuwa Mkurugenzi wake, Dk Idris Rashidi, ilitahadharisha kamati hiyo kwamba utafiti uliofanywa na wataalamu umegundua kwamba kama hatua za haraka hazitachukuliwa , taifa litakabiliwa na tatizo la mgawo wa umeme.

Tanesco pia iliitahadharisha serikali kutafakari uwezekano wa kampuni binafsi kujitokeza na kununua mitambo hiyo na kisha kuliuzia shirika hilo umeme.

Desemba 15 mwaka 2008, Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge ilikataa kuunga mkono uamuzi wa Tanesco kununua mitambo ya Dowans ikisema kuuridhia ilikuwa ni kukiuka utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na Bunge Februari mwaka 2007 kuhusu kampuni za Richmond na Dowans.

Pia kamati hiyo ilikataa kujihusisha na jambo hilo ikijua kuwa kufanya hivyo ni kuvunja Kanuni ya 53 (8) na 54 (4) za Kanuni za Kudumu za Bunge (toleo la 2007), ambazo zote zinakataza kurudiwa kwa mjadala wa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi na Bunge.

Siku moja tu baada ya Kamati hiyo iliyochini ya mbunge wa Jimbo la Bumbulu William Shellukindo kutoa tamko hilo, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alitangaza uamuzi wa serikali kukubaliana na hatua ya kusitisha nia yake ya kutaka kununua mitambo hiyo ya Dowans.

No comments:

Post a Comment