WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Tuesday, June 1, 2010

Wahindi Walalamikia Ukubwa wa Kondomu


Utafiti uliofanyika nchini India umeonyesha kuwa wanaume wengi nchini India hawafurahishwi na ukubwa wa kondomu unaotambulika duniani kwakuwa kondomu hizo ni kubwa sana kulinganisha na ukubwa wa nyeti zao.
Utafiti huo uliowashirikisha wanaume 1,000 wa nchini India ulionyesha kuwa kondomu zenye ukubwa unaotambulika kimataifa huwapwaya wanaume wengi wa nchini India.

Utafiti huo uliweka wazi kuwa zaidi ya nusu ya wanaume walioshiriki utafiti huo walikuwa na uume ambao ulikuwa ni mfupi kulinganisha na ukubwa wa kondomu.

Utafiti huo uliofanyika kwa miaka miwili uliweka wazi kuwa asilimia 60 ya wanaume nchini India wana uume wenye urefu kati ya sentimeta tatu hadi tano pungufu ya ukubwa wa kondomu unaotambulika duniani.

Matokeo ya utafiti huu yamepelekea makampuni ya kutengeneza kondomu nchini India yatakiwe kutengeneza kondomu zenye ukubwa tofauti tofauti.

Matokeo ya utafiti huu yametiliwa mkazo kwakuwa India ndiyo nchini inayoongoza duniani kwa idadi kubwa ya watu walioathirika na virusi vya Ukimwi.

KIJANA AGONGWA NA TRENI JIJINI DAR


Mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amegongwa na treni katika eneo la Keko darajani jijini Dar es Salaam.
Mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amegongwa na treni katika eneo la Keko darajani jijini Dar es Salaam, kijana huyo inasadikika alikuwa akiishi chini ya daraja hilo ambapo kuna njia ya reli .

Kwa kuwa reli hiyo ilikuwa haitumiki kwa muda mwingi kijana huyo aliamua kufanya sehemu ya kulala leo serikali ya Tanzania ilitangaza kuwa safari ya treni ya kuelekea Kigoma , mwanza, mpanda itaanza baada ya matengenezo ya daraja lililokuwa limeharibika kutengenezwa,

Bila kujua kama kuna mtu tayari kichwa cha treni kilipita katika njia yake huku jamaa akiwa amepitiwa na usingizi katika reli na kukanyagwa hadi kufa.

Hadi tunakwenda mitaamboni hakuna taarifa za uhakika za kijana huyo ambaye amegongwa majira ya asubuhi leo.

Watanzania Kuzilipa Gharama za Kuwaleta Wabrazili


Washabiki wa soka Tanzania ndio wataolazimika kujipinda ili kuzilipa dola milioni 2.5 ambazo Brazili imelipwa ili kuileta timu yake Tanzania.
Shirikisho la soka Tanzania, TFF limepanga viingilio vikubwa kwenye mechi kati ya Brazili na Tanzania itakayofanyika jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam.

Viingilio vimekuwa vikubwa kuliko kawaida ili kulipia gharama za kuwaleta mastaa wa Brazili Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vingi vya habari, Tanzania imewalipa Brazili dola milioni 2.5 ingawa TFF imekataa kusema imewalipa Brazili dola milioni ngapi.

TFF ilisema kuwa kuwaleta Brazili nchini Tanzania ni gharama sana hivyo Watanzania wajiandae kukaza mikanda kulipa gharama hizo.

TFF inaamini kuwa mapato ya magetini yatatosha kuzilipa gharama za kuwaleta Brazili Tanzania.

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa juni 7 vimepangwa kuanzia Tsh. 30,000 hadi Tsh. 200,000.

Majukwaa ya VIP tiketi zinaanzia laki moja hadi laki mbili ambapo taarifa za TFF zinasema kuwa tiketi za laki mbili zimeishanunuliwa zote.

Majukwaa yaliyobakia tiketi zinaanzia Tsh. 30,000 hadi Tsh. 80,000.

BAJETI YA TANZANIA MWAKA UJAO NI TRILIONI 11


SERIKALI ya Tanzania imepanga kutumia Shilingi trilioni 11.1 katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2010/11.
Bajeti hiyo imeongezeka shilingi trillion 1.6 ukilinganisha na ya mwaka jana wa fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Uchumi , Mustapha Mkulo, alisema kati ya fedha hizo, zinazotarajiwa kukusanywa ni Sh trilioni 6 ambazo ni za mapato ya ndani na Sh trilioni 2.8 misaada na mikopo kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Alisema pia kati ya fedha hizo, Sh trilioni 1.1 ni mikopo ya ndani, Sh bilioni 983.7 mikopo ya masharti ya kibiashara na Sh bilioni 30 ni mapato kutokana na ubinafsishaji.

Mkulo alisema katika bajeti hiyo, kilimo, huduma za jamii kama elimu, afya na maji, ardhi na umwagiliaji, miundombinu ambayo ni reli, bandari, viwanja vya ndege na nishati ndio vitapewa vipaumbele.

Bajeti hiyo inatarajiwa kutumia Sh trilioni 7.8 kwa matumizi ya kawaida na Sh trilioni 3.2 kwa matumizi ya maendeleo.

Hata hivyo, alisema Serikali itaendelea kutumia mikopo nafuu na kuanzia mwaka ujao itatumia mikopo ya kibiashara kwa ajili ya kugharimia bajeti yake.

Aidha, alisema kwa mwaka wa fedha 2010/11 Serikali inatarajia kukusanya mapato ya ndani yasiyopungua Sh trilioni sita, sawa na asilimia 17.3 ya pato la Taifa ikilinganishwa na mapato ya asilimia 16.4 ya pato la Taifa ya mwaka jana.

Pia alisema Serikali inatarajia kukusanya Sh bilioni 1.7 kutoka kwenye vyanzo vya halmashauri ambapo pia imelenga kuendeleza mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani, kuimarisha usimamizi na udhibiti wa makusanyo, kuchukua hatua za kupunguza misamaha ya kodi, kutenga fedha kwa ajili utekelezaji wa kaulimbiu ya Kilimo Kwanza.

AMPENDA DADA YAKE, AKAAMUA KUMUONA

Mwanaume mmoja nchini Ireland amejikuta akimzalisha dada yake bila kutarajia baada ya kuangukia kwenye mapenzi bila kujua kuwa mwanamke huyo ni dada yake. Ameamua kufunga naye ndoa ili waweze kumtunza mtoto aliyezaa naye.
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Mark wa nchini Ireland alijikuta akizaa na dada yake wa baba mmoja mama tofauti, baada ya kuanza naye uhusiano bila kufahamu kuwa ni dada yake.

Wazazi wa Mark waliachana wakati Mark akiwa mdogo sana ambapo kwa jinsi ndoa hiyo ilivyovunjika kwa mgogoro mkubwa mahakamani, Mark alipewa jina tofauti la baba na mahakama iliamuru mtoto huyo asiambiwe baba yake anaitwa nani.

Kasheshe liliibuka baada ya Mark kukutana na mwanamke disco katika mji tofauti na anaoishi. Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Maura naye alienda kwenye disco hilo akitoka kwenye mji mwingine tofauti.

Mark alianza uhusiano wa kimapenzi na Maura wakati huo. Miaka miwili baadae Maura alipopata ujauzito ndipo wawili hao walipoamua kuishi pamoja.

Baada ya Maura kujifungua, Mark aliamua kumtambulisha Maura kwa mama yake na ndipo ukweli ulipofichuka.

Mama yake Mark alimuuliza Maura baba yake anaitwa nani, alipolitaja jina lake ndipo mama huyo alipomwambia Mark "Mwanangu huyo ni dada yako".

Matokeo ya vipimo vya DNA yaliyotolewa mwezi uliopita yalithibitisha kuwa Mark na Maura ni mtu na dada yake.

Hata baada kugundua kuwa uhusiano wao ni haramu, wawili hao wameamua kuuendeleza na wamepanga kuzaa watoto wengi zaidi.

"Najua watu watatufikiria vibaya, kama tusingekuwa na mtoto tungeweza kufikiria kusitisha uhusiano wetu lakini kwakuwa tuna mtoto mmoja, tutafunga ndoa tuzae watoto wengi zaidi", alisema Mark.

Mark na Maura wanatoa lawama zao kwa mfumo wa sheria ambao ulizuia Mark kumjua baba yake.

Wamepanga kumfungulia kesi ya fidia jaji aliyeamuru Mark asijulishwe baba yake.