WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Wednesday, April 28, 2010

OBAMA NA AGA KHAN WAGUSWA NA MUUNGANO TANZANIA



RAIS Barack Obama wa Marekani na Aga Khan Kiongozi wa wa Ismailia duniani wamemtumia Rais Jakaya Kikwete salamu za pongezi kwa kwa kusherehekea sikukuu ya Muungano iliyoadhimishwa jana nchini kote.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana ikinukuu taarifa ya ubalozi wa Marekani hapa nchini ilielezea kuwa salamu hizo kutoka kwa viongozi hao zilitumwa jana.

“Mpendwa Rais, kwa niaba ya watu wa Marekani, nakutumia salamu zangu za dhati kukupongeza wewe na watu wa Tanzania, wakati mnaposherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26, April,” ilieleza sehemu hiyo ya taarifa iliyopitia Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

“Ni matumaini yangu kwamba miaka ijayo italetea Watu wa Tanzania Amani na mafanikio ya kudumu,” Rais Obama alimueleza Rais Kikwete katika salamu hizo na kuelezea nia yake na matarajio ya baadaye kuwa nchi hizo zitaimarisha mahusiano baina yao.

“Natarajia tutaimarisha na kuwa na mahusiano thabiti baina ya nchi zetu,” salamu za Rais Obama ilieleza.

Naye Kiongozi wa wa Ismailia duniani alimueleza Rais Kikwete furaha yake na kutoa salamu za heri kwa Rais Kikwete na Watanzania wote.

“Wa-Ismailia Imamat na Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, kwa pamoja tunaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania na Jumuiya za Kiraia katika kuchangia katika ukuaji wa nchi na nafasi kwa watu wote wa Taifa,” alieleza na kumshukuru Rais Kikwete kwa ushirikiano wake.

“Tunathamini ushirikiano wako na wa Serikali yako katika kuunga mkono na kutia moyo shughuli za Jumuiya ya Aga Khan,” Salamu za Aga Khan zilielezea.

Jana maelfu ya watu walioenda kushuhudia sherehe za maadhimisho ya Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walionyesha hisia zao wakati marais wastaafu, Ali Hassani Mwinyi na Benjamini Mkapa walipoingia.

Umati huo ulilipuka shangwe za kelele na vifijo wakati viongozi hao walipoingia kwenye uwanja huo mkongwe kwa nyakati tofauti kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuingia na kuzunguka uwanja mzima akipunga mkono.

Mkapa, ambaye aliongoza serikali ya awamu ya tatu ambayo ilijipatia sifa ya kuinua uchumi na kuboresha miundombinu, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia uwanjani katika siku hiyo iliyokuwa na jua la vipindi.

Baada ya Mkapa, ambaye aliongoza nchi kwa sera aliyoiita ya "ukweli na uwazi", kuingia uwanjani hapo kwa gari la kifahari aina ya Range Rover (Vogue), kelela za shangwe na vigelegele zililipuka kutoka kwenye umati wa watu.

Mkapa aliyeingia uwanjani hapo majira ya saa 3:15 alipishana kwa takriban dakika 15 na kiongozi wa serikali ya awamu ya pili, Mwinyi ambaye pia aliamsha kelele za shangwe kutoka kwa watu waliohudhuria.

Kama ilivyokuwa kwa Mkapa, Mwinyi ambaye aliingia uwanjani hapo na gari aina ya Toyota Landcruiser (VX) alishangiliwa kwa nguvu tofauti na ilivyokuwa kwa viongozi wa serikali ya sasa, akiwemo Rais Kikwete.

WAALIMU WAWILI WAUAWA KWA RISASI TARANGIRE

WALIMU wawili wa Shule ya Msingi ya Tarangire mkoani Manyara, Joyce Paulo, 30, na Anna Nkya, 24, wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori kutoka Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kutokana na kilekilichoelezwa kuwa niugomvi wa mapenzi.

Imeelezwa kuwa askari aliyefanya mauaji hayo alikuwa lindoni kwenye hifadhi hiyo, lakini akaamua kuacha kazi yake na kwenda hadi nje ya hifadhi kutekeleza mauaji hayo ya mtu anayesadikiwa kuwa ni mkewe na mgoni wake.

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la Tarangire lililo kwenye Kata ya Ngaiti baada askari huyo, ambaye ametajwa kuwa ni Paulo Keregesi kuvamia nyumba waliokuwa wanaishi walimu hao na kuwamiminia risasi zilizokatisha maisha yao.

Diwani wa Kata ya Ngaiti inayopakana na hifadhi hiyo, Olais Ole Koine alisema kabla ya mauaji hayo, Keregesi alikuwa ametengana na mkewe Joyce, ambaye mwalimu na ambaye amezaa naye watoto wawili.

Diwani huyo alisema taarifa ambazo wamepata mara baada ya mauaji hayo zinaeleza kuwa askari huyo na mkewe Joyce ambao wote ni wenyeji wa mkoani Mara walikuwa na ugomvi kwa takriban miezi miwili iliyopita.

Alisema, hata hivyo, walikwenda nyumbani kwao kusuluhishwa lakini waliporudi mwanamke huyo hakurejea kwa mumewe anayeishi ndani ya hifadhi hiyo na akaamua kuishi na mwalimu mwenzake nje ya hifadhi hiyo.

"Baada ya hali hiyo ndio juzi majira ya saa 3:00 usiku askari huyo aliyekuwa lindoni na silaha alivamia nyumba ya walimu na kwa kupitia dirishani aliwapiga risasi na wakafariki papo hapo na baadaye akatoweka," alisema Diwani Koine.

Alisema wamepata taarifa kuwa askari huyo aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 aliiterekeza eneo la Mdori na kukimbia na baadaye alituma ujumbe mfupi wa simu kueleza kuwa anahusika na mauaji hayo na kwamba ameiacha pikipiki mjini Babati.

"Muda huu tunajiandaa kuja Arusha ili kupanga taratibu za kusafirisha marehemu kwani Mwalimu Nkya ni mwenyeji wa Machame na Joyce ni mwenyeji wa Serengeti," alisema Diwani Koine.

Polisi mkoani Manyara wamethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na wanamsaka askari huyo. Mkuu wa hifadhi ya Tarangire, Erastus Lufungulo, ambaye kwa sasa yupo likizo, pia amethibitisha kupata taarifa za mauaji hayo.
"Naomba uwasiliane na mkurugenzi mkuu wa Tanapa kama kuna maelezo mnahitaji kuhusu huyo askari," alisema Lufungulo.

Hata hivyo, meneja uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete alisema jana kuwa bado hawajapata taarifa kamili za tukio hilo na aliomba kupewa muda zaidi ili atoe maelezo zaidi.

ZAIDI YA WAFUNGWA 3000 WAACHIWA HURU

RAIS Jakaya Kikwete, ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3,101 waliuokuwa wanatumikia vifungo kwenye magereza mbalimbali nchini.

Rais alitoa msamaha huo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wafungwa walionufaika na msahama huo ni waliokuwa wanatumikia vifungo visivyozidi miaka mitano jela, wengine ni wafungwa wenye magonjwa kama ya Ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wanaelekea kuwa katika siku za mwisho za maisha yao, baada ya kuthibitishwa na jopo la wataalamu wea afya ngazi ya wilaya na mkoa.

Wengine ni wazee wenye umri wa miaka 70 na zaidi, wakiwemo wajawazito, wanawake wenye watoto wanaonyonya, walemavu wa mwili na akili pia.

Msamaha huo hautawahusu wafungwa wanaotokana na makundi ya waliohukumiwa kunyongwa, wenye makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, kupokea na kutoa rushwa, unyang'anyi wa kutumia silaha, ubakaji, kunajisi, kulawiti na wizi wa magari kwa kutumia silaha.

Wengine ambao hawatanufaika na msamaha huo ni wale waliowapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na kusababisha washindwe kuendelea na

NVUA KUBWA YALETA BALAA DAR


JANA jiji la Dar es salaam lilitawaliwa na shida na mapungungufu makubwa katika huduma mbalimbali kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku nzima hali iliyofanya wakazi wa jiji kuteseka kutokana na hali hiyo.
Mbali na kuwa na dmapungufu katika huduma nyingine tofautitofauti shida kubwa zaidi ilikuwa ni upande wa usafiri ambao ulikuwa haupatikani kutokana na mvua hiyo.


NIFAHAMISHE ilishuhudia makundi ya watu yakihaha huku na huku, na yakipita barabarani mithili ya maandamano yakitembea kwa miguuu kurudi majumbani mwao kwa kukoseskana kwea huduma hiyo.


Hali hiyo ilidumu siku nzima katika kila kituo cha mabasi jijini ambapo mabasi yalikuwa hayafiki mjini na wakazi hao kulazimika kurudi kwa miguu majumbani mwao.


Jopo la waandishsi wa nifahamishe nao dhahama hiyo iliwakumba kwa kile kilichowakuta wamefika kituoni Posta majira ya saa 11 ya jioni na hadi ilipofika majira ya saa moja kasorobo hawajapata usafiri na kulazimika watembee kwa miguu kuhamia katika kituo cha nyuma cha Akiba na hali ilikuwa hivyohivyo.

Hali ilivyozidi kuwa tata zaidi waliamua warudi nyuma na kuelekea kituo cha fire ili waweze kupata usafiri na wageuze na mabasi lakini hali hiyo walidumu nayo kwa takribani dakika 45 kituoni hapo bila kuwa na dalili yoyote ya kupata usafiri.

Hiyo ndiyo hali iliyokuwa jana katika jiji la Dar es Salaam kwa wakazi wengi waishio humo wakionekana kurudi kwa miguu kutokana na adha iliyokuwepo

Mapacha Wenye Mguu Mmoja Wanavyowasilimisha Wanakijiji


apacha Pheinbom na Shevoboh wa nchini Cameroon walipozaliwa wakiwa wameungana kuanzia kifuani kushuka chini, wanakijiji waliwaona ni kama mkosi mkubwa kwa jamii lakini baada ya mapacha hao kutenganishwa na madaktari wa Saudi Arabia, mapacha hao wamebadilisha maisha ya wanakijiji na wanakijiji wengi wanabadili dini kuwa waislamu.
Mapacha Pheinbom na Shevoboh walipozaliwa wakiwa wameungana walionekana kama mkosi lakini baada ya kutenganishwa na madaktari wa Saudi Arabia, maisha yao yamebadilika na wamefanikiwa kuwa chachu ya mabadiliko ya maisha katika kijiji chao.

Walipozaliwa wakiwa wameungana kuanzia kifuani kushuka chini, madaktari wa uzazi katika hospitali ya Babanki Tungo, kaskazini magharibi mwa Cameroon waliikimbia Hospitali kutokana na mshtuko wa uzazi huo wa aina yake kijijini hapo.

Baadhi ya wanakijiji waliamini kuwa watoto hao ni adhabu toka kwa mungu kwa baba wa watoto hao ambaye alikuwa na wake wawili na jumla ya watoto 13.

Wanakijiji wengine waliamini kuwa watoto hao ni fimbo ya adhabu kwa kijiji kizima kwani siku chache baada ya kuzaliwa kwa watoto hao mkuu wa kijadi wa kijiji hicho aliuliwa kwa kuchomwa moto akiwa hai na wanakijiji wenye hasira.

Hali ilibadilika baada ya mfalme wa Saudia kukubali kulipa gharama za kuwatenganisha watoto hao mapacha wa kike.

Baada ya operesheni ya masaa 16 iliyofanyika nchini Saudia, madaktari walifanikiwa kuwatenganisha mapacha hao na hivi sasa kila mmoja ana tumbo lake mwenyewe isipokuwa wamebaki na mguu mmoja mmoja.

Ikiwa ni miaka mitatu tangia operesheni hiyo ilipofanyika, mapacha hao wanajiandaa kwenda tena Saudi Arabia kufundishwa jinsi ya kutumia miguu ya bandia kutembea kama watu wengine.

Kijiji cha Babanki Tungo awali kilikuwa ni kijiji kilichojaa waumini wengi wa kikristo lakini hivi sasa hali imebadika baada ya serikali ya Saudi Arabia kuamua kujenga hospitali, shule ya msingi, shule ya chekechea pamoja na kituo cha kiislamu kwenye kijiji hicho.

Wazazi wa mapacha hao ndio waliokuwa wa kwanza kubadili dini na wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa mafundisho ya dini ya waislamu yaliyopelekea kusilimu kwa wanakijiji wengi.

Wazee wa kijiji wanahofia kuwa kijiji hicho ambacho awali kilikuwa ni cha kikristo kidogo kidogo kinaanza kubadilika kuwa kijiji cha kiislamu.

Baba wa mapacha hao ambaye awali alikuwa akiitwa Ngong James Akumbu, hivi sasa anaitwa "Abdallah", wakati mama yao aliyeitwa Emerencia hivi sasa anaitwa "Aisha".

"Kabla ya shule kufunguliwa, nilikuwa sina kazi, nilikuwa na wapenzi wengi na nilikuwa mlevi", alisema mwalimu Kum Edwin ambaye naye amebadili dini na hivi sasa anaitwa "Abdallah Wagf".

"Hivi sasa sinywi tena pombe na nimeamua kutafuta mwanamke wa kuoa kwasababu kuwa na wapenzi wengi si tabia nzuri", aliongeza mwalimu Edwin.

"Hivi sasa watu wa kijiji cha Babanki Tungo wanawaona mapacha Pheinbom na Shevoboh kama baraka toka kwa mungu na sio mkosi kama tulivyofikiria awali", alimalizia kusema mwalimu Edwin.

KORTINI KWA UTAPELI ETI WANAO UWEZO WA KUMFUFUA MTU

WAKAZI wawili wa Jiji la Dar es Salaam, wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu baada ya kudai wana uwezo wa kumfufua mtoto aliyekufa na kudai hakufa kihalali.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jana, na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka wa Polisi, Nassoro Sisiwaya mbele ya Hakimu Suzane Kihawa wa mahakama hiyo.

Sisiwaya alidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja walijipatia fedha taslimu za kitanzania Shilingi milion 3.6 kutoka kwa Amina Juma kwa makubaliano kwamba wana uwezo wa kumfufulia mtoto aliyekufa wa mlalamikaji huyo.

Alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo, Mei 5 mwaka jana katika eneo la Kimara Baruti na kwamba walidai wana uwezo wa nguvu za kichawi za kuweza kumfufua marehemu huyo na kumrudisha akiwa hai.

Washtakiwa hao ni Shabani Juma (46), mkazi wa Tandale kwa Tumbo ambaye ni mganga wa jadi na Godfrey Zakaria (26) mkazi wa Tandale fundi wa umeme wa magari wote walimuahidi mama huyo kuwa mtoto huyo angefufuka kwa kuwa hakufa kihalali.

Ilidaiwa upelelezi wa shauri hilo umeisha kamilika na kesi itaanza kusikilizwa Mei 17 mwaka huu.

Washtakiwa wako nje kwa dhamana.

THE DEATH OF OUR BELOVED FATHER JOHN IBRAHIM KADIGI


MR. MR. JOHN IBRAHIM KADIGI of Ngudu Mwanza/Morogoro, left his walk of life at the age of 84 on April 21, 2010 at SAIFEE Hospital in Mumbai India, where he went for medical treatment. He survived by his wife Ruth. Sons - Julius and Methuselah/Fimbo. Daughters - Mary, Stelah Mngodo, Eunice, Jane, Katherine, Hellen Mwaituka and Happy Holm. Grandchildren - Jeff, John, James, Jeremiah, Junior, Hellen and David. The family is still on arrangements for taking his body from India to Tanzania for burrial. He will be greatly missed by all his family and friends.

The memorial and fundraising service took place on Sunday April 25, 2010 at 2970 Lorna Rd, Birmingham AL 35216, at 3:00 - 5:00pm. Below are the numbers of what we have raised so far.

OUR GOAL IS TO RAISE $4,000

CHECKS COLLECTED $1,135
CASH COLLECTED $ 540
TOTALS $1,675

WE STILL NEED $2,325

Below are bank accounts information that you can use for sending your donation

BANK NAME: REGIONS BANK
ACCOUNT NO: 0106703879

BANK NAME: WACHOVIA / WELLS FARGO BANK
ACCOUNT NO: 8453467477

For the word of comforty please visit the family at 1106 Colonial Dr. Alabaster AL 35007 or call the Kadigis at (205) 664 - 1197
Job 1:21 "Naked I came from my mother's womb, and naked I will depart. The LORD gave and the LORD has taken away; may the name of the LORD be praised."

If you have any question or you need some more information please write to us at admin@themissionband.org or call

REV. FRED MWAITUKA - (205) 919 - 9978
REV. DEO LUBALA - (205) 477 - 1361
ISACK MAYALA (205) 267 - 2137 of Ngudu Mwanza/Morogoro, left his walk of life at the age of 84 on ApIGIril 21, 2010 at SAIFEE Hospital in Mumbai India, where he went for medical treatment. He survived by his wife Ruth. Sons - Julius and Methuselah/Fimbo. Daughters - Mary, Stelah Mngodo, Eunice, Jane, Katherine, Hellen Mwaituka and Happy Holm. Grandchildren - Jeff, John, James, Jeremiah, Junior, Hellen and David. The family is still on arrangements for taking his body from India to Tanzania for burrial. He will be greatly missed by all his family and friends.

The memorial and fundraising service took place on Sunday April 25, 2010 at 2970 Lorna Rd, Birmingham AL 35216, at 3:00 - 5:00pm. Below are the numbers of what we have raised so far.

OUR GOAL IS TO RAISE $4,000

CHECKS COLLECTED $1,135
CASH COLLECTED $ 540
TOTALS $1,675

WE STILL NEED $2,325

Below are bank accounts information that you can use for sending your donation

BANK NAME: REGIONS BANK
ACCOUNT NO: 0106703879

BANK NAME: WACHOVIA / WELLS FARGO BANK
ACCOUNT NO: 8453467477

For the word of comforty please visit the family at 1106 Colonial Dr. Alabaster AL 35007 or call the Kadigis at (205) 664 - 1197
Job 1:21 "Naked I came from my mother's womb, and naked I will depart. The LORD gave and the LORD has taken away; may the name of the LORD be praised."

If you have any question or you need some more information please write to us at admin@themissionband.org or call

REV. FRED MWAITUKA - (205) 919 - 9978
REV. DEO LUBALA - (205) 477 - 1361
ISACK MAYALA (205) 267 - 2137