SHIRIKISHO la Vyama vya wafanyakazi nchini {TUCTA] umetangaza mgomo utakaofanyika nchi nzima kuaninzia Mei 5, mwaka huu kupinga mambo mbalimbali serikalini. Nacho Chama cha Walimu Tanzania [CWT] umeunga mgomo huo na umesema utashiriki ipasavyo na wameheshimu kauli ya tucta kwa kuwa ina nguvu na wanakusudia kugoma hadi hapo haki zao zitakapotekelezwa ipasavyo.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kwa sasa anatoa taarifa kwa walimu wote nchini na wanatakiwa wafahamu kuwa chama chao kimeitikia wito wa kushiriki kwenye mgomo wa kudai mambo mbalimbali ambayo serikali imeyadharau kwa muda mrefu.
Aliongeza kuwa viongozi wa vyama vyote wamekubaliana kuwatangazia wanachama wao kuhusu mgomo huo ili washirikiane kudai haki zao chini ya mwavuli wa Tucta.
Mgomo huo unakusudia madai ya mishahara duni isiyokidhi mahitaji, mafao duni ya wastaafu kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na ulipishwaji wa kodi kubwa kwenye mishahara midogo wanayopata wafanyakazi.
Tucta imedai kuwa siku ya kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi Mei Mosi watajadili kindani jinsi ya kuanza kufanya mgomo huo kwa kuw wafanyakazi wote hukutana siku hiyo.
Monday, March 22, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment