WELCOME TO TANZAMERICA'S WORLD

Tanzamerica
Is a social network page that updates you with current news from Tanzania , America and around the world. Also, gives you the opportunity to link up your business or ministry between Tanzania and America .We are also dealing with Entertainments (music,movie and art) news, and sports between the two country.
For more info on how to advertise your business, ministry, career and news
Contact us:
+1360 561 6629
Patrick.
tanzamerica@gmail.com
info@patricknworld.com
http://www.tanzamerica.blogspot.com
Detailed Info

http://www.celebafrica.blogspot.com
http://www.patricknworld.blogspot.com
http://www.reverbnation.com/patricknewman

Wednesday, April 28, 2010

Mapacha Wenye Mguu Mmoja Wanavyowasilimisha Wanakijiji


apacha Pheinbom na Shevoboh wa nchini Cameroon walipozaliwa wakiwa wameungana kuanzia kifuani kushuka chini, wanakijiji waliwaona ni kama mkosi mkubwa kwa jamii lakini baada ya mapacha hao kutenganishwa na madaktari wa Saudi Arabia, mapacha hao wamebadilisha maisha ya wanakijiji na wanakijiji wengi wanabadili dini kuwa waislamu.
Mapacha Pheinbom na Shevoboh walipozaliwa wakiwa wameungana walionekana kama mkosi lakini baada ya kutenganishwa na madaktari wa Saudi Arabia, maisha yao yamebadilika na wamefanikiwa kuwa chachu ya mabadiliko ya maisha katika kijiji chao.

Walipozaliwa wakiwa wameungana kuanzia kifuani kushuka chini, madaktari wa uzazi katika hospitali ya Babanki Tungo, kaskazini magharibi mwa Cameroon waliikimbia Hospitali kutokana na mshtuko wa uzazi huo wa aina yake kijijini hapo.

Baadhi ya wanakijiji waliamini kuwa watoto hao ni adhabu toka kwa mungu kwa baba wa watoto hao ambaye alikuwa na wake wawili na jumla ya watoto 13.

Wanakijiji wengine waliamini kuwa watoto hao ni fimbo ya adhabu kwa kijiji kizima kwani siku chache baada ya kuzaliwa kwa watoto hao mkuu wa kijadi wa kijiji hicho aliuliwa kwa kuchomwa moto akiwa hai na wanakijiji wenye hasira.

Hali ilibadilika baada ya mfalme wa Saudia kukubali kulipa gharama za kuwatenganisha watoto hao mapacha wa kike.

Baada ya operesheni ya masaa 16 iliyofanyika nchini Saudia, madaktari walifanikiwa kuwatenganisha mapacha hao na hivi sasa kila mmoja ana tumbo lake mwenyewe isipokuwa wamebaki na mguu mmoja mmoja.

Ikiwa ni miaka mitatu tangia operesheni hiyo ilipofanyika, mapacha hao wanajiandaa kwenda tena Saudi Arabia kufundishwa jinsi ya kutumia miguu ya bandia kutembea kama watu wengine.

Kijiji cha Babanki Tungo awali kilikuwa ni kijiji kilichojaa waumini wengi wa kikristo lakini hivi sasa hali imebadika baada ya serikali ya Saudi Arabia kuamua kujenga hospitali, shule ya msingi, shule ya chekechea pamoja na kituo cha kiislamu kwenye kijiji hicho.

Wazazi wa mapacha hao ndio waliokuwa wa kwanza kubadili dini na wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa mafundisho ya dini ya waislamu yaliyopelekea kusilimu kwa wanakijiji wengi.

Wazee wa kijiji wanahofia kuwa kijiji hicho ambacho awali kilikuwa ni cha kikristo kidogo kidogo kinaanza kubadilika kuwa kijiji cha kiislamu.

Baba wa mapacha hao ambaye awali alikuwa akiitwa Ngong James Akumbu, hivi sasa anaitwa "Abdallah", wakati mama yao aliyeitwa Emerencia hivi sasa anaitwa "Aisha".

"Kabla ya shule kufunguliwa, nilikuwa sina kazi, nilikuwa na wapenzi wengi na nilikuwa mlevi", alisema mwalimu Kum Edwin ambaye naye amebadili dini na hivi sasa anaitwa "Abdallah Wagf".

"Hivi sasa sinywi tena pombe na nimeamua kutafuta mwanamke wa kuoa kwasababu kuwa na wapenzi wengi si tabia nzuri", aliongeza mwalimu Edwin.

"Hivi sasa watu wa kijiji cha Babanki Tungo wanawaona mapacha Pheinbom na Shevoboh kama baraka toka kwa mungu na sio mkosi kama tulivyofikiria awali", alimalizia kusema mwalimu Edwin.

No comments:

Post a Comment